Sekoutoure Khalifa Mndeme 
(24 Julai 1965 – 10 Julai, 2011)

Tarehe 10 Julai, 2011 Sekoutoure ‘Toure’ Khalifa mzawa wa Usangi, Wilaya ya Mwanga, mkazi wa Kunduchi-Mtongani, Dar es Salaam, aliaga dunia katika Hospitali ya Apollo, nchini India.

Jamii ilitoa msaada mkubwa tangu pale Toure alipolazwa Hospitali ya Aga Khan mwishoni mwa Juni, baadaye akahamishiwa Taasisi ya MOI (Muhimbili) na kisha kupelekwa India kwa uchunguzi zaidi na matibabu, hadi alipofariki. Tuliendelea kupata ushirikiano wenu hadi mwili wa Toure ukarejeshwa Dar trh toka India 13 Julai na hatimaye kusafirishwa kwenda Usangi–Ngujini kwa mazishi, Ijumaa, trh 15 Julai, 2011.

Familia ya Sultani na Omari Muyanza ya Usangi Mwanga, ya Hemedi Mwamtemi ya Lushoto na ile ya Toure (mjane Halima H. Mwamtemi, wanawe Khalifa (16), Hemedi (13) na Bi Hafsa “Doctor” (6) walinufaika na kufarijika mno kwa upendo na ushirikiano wa ninyi ndugu, jamaa, majirani na marafiki.

Kwa vile sio rahisi kuwashukuru mmoja-mmoja, mamia ya watu na taasisi, mliotuliwaza na kutusaidia kwa hali na mali katika kipindi cha majonzi makuu, tunawaomba, kwa moyo mkunjufu, mpokee ujumbe huu kama tamko letu la kusema: “AHSANTENI SANA. Mwenyezi Mungu awabariki na kuwazidishia neema.”

Hata hivyo, twaomba kutoa shukrani mahsusi kwa hawa wachache wafuatao: CRDB Bank (Tawi la Vijana), Utawala na wafanyikazi wa CRDB Bank Makao Makuu na kwingine nchini, Hospitali ya Aga Khan (DSM), Dr Rutta and Dr Nchembe wa Taasisi ya MOI, Utawala na Wafanyikazi wa Tanzania Postal Bank, Hospitali ya Apollo (India), Real Insurance, Utawala na Wafanyikazi wa Mwanga Community Bank, Tanzania Professionals Network, Gymkhana Club, Break Point, Family Social Club, Feza Boys Sec School, Valentine and Women Group Kunduchi, Masjid Taqwa ya Kunduchi na Masjid Ngujini ya Usangi.

Shukrani rasmi pia ziwafikie: Mhe. Cleopa D Msuya, Mhe. Prof Jumanne Maghembe, Mhe. Bernard Membe, Mhe. Mecky Sadiki, Bw Lawrence Masha, Sheikh Meraji Msoffe, Bw na Bi R. Manumba, Bw na Bi S. Kova, Bw na Bi s Alex Lema, Bw na Bi Eidriss Mavura, Ambassador Herman Mkwizu, Colonel Martin Mwankanye, Bw M. I. Michuzi, Bw Amin Mcharo, Bw George Mbati, Bw T. Kejo, Bw Stephen Kilindo, Bw Pius Kassuga, Bw R. Mringo, Balozi Fadhili Mbaga, Bw Stephen Kilindo, Bw Kwame Ghadhal, Bw Eric Shigongo and Bw Richard K. Muzo.

Shukrani za kipekee pia ziende kwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na hasa-hasa issamichuziblogspot.com and globalpublishertz.com, ambavyo vilifanya kazi kubwa kuiarifu jamii juu ya kifo, maziko na mazishi ya Toure.

Sekoutoure alikuwa mtoto wa tatu wa hayati Khalifa Sultani Muyanza na Bi Mwezine Joho. Alikuwa kaka wa hayati Leda, Bi Mwajuma, hayati Dr Joho, Bi Mariam, Bw Omari na Bw Segoh.

Toure; ni kweli kwamba umetutoka kimwili, lakini utabaki ndani ya mioyo yetu daima. Upendo, ucheshi hekima na busara zako zitabaki kama dira na changamoto ya kuwania ubora kwa sote ulotuacha nyuma.

“INNA LILLAH wa Ina ILLAYH RAJ’UNN – Kwa Mola tumetoka na Kwake tutarejea.” - Al Quran, Sura 6:128

MOLA NA AILAZE ROHO YA SEKOUTOURE PEMA PEPONI - AMINA.

HITMAya Sekoutoure na ile ya mpwawe, Sheni Sultani ( 1977 -10 Julai, 2011) itasomwa Jumamosi, Sept 17, 2011, kuanzia saa 7 mchana, nyumbani kwake Kunduchi-Mtongani. 

KARIBUNINYOTE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...