Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wa familia 70 wa Kisiwani Piki na Mzambaraun i Takao,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni,akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliofiwa na jamaa zao katika kisiwa cha Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha wageni alipowasili katika skuli ya Piki, kuzungumza na wananchi wa familia 70 wa Kisiwani Piki na Mzambarauni Takao,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni,akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliofiwa na jamaa zao katika kisiwa cha Pemba.
Waziri wa Ardhi,Makaazi,maji na Nishati, Mhe. Ali Juma Shamuhuna,akiwapa pole wananchi wa Mtambwe Daya waliofiwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,iliyozama katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja wakati ikielekea Pemba,hivi karibuni.
Baadhi ya wananchi wa familia 70 wa Kisiwani Piki na Mzambarauni takao,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein alipofika Skuli ya sekondari ya Piki, kuwapa pole,kutokana na ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander hivi karibuni . Picha na Ramadhan Othman Pemba
Kaka Michuzi, hii picha ya tatu kutoka chini naona haiendani na maelezo. Maana aliyesimama nina hakika si mke wa Mheshimiwa Shein. Na mbali ya hicho kiremba au hijabu hakuna mwanamke kwenye hiyo picha! Naamini kaka Michuzi shughuli ni nyingi, ila uwaambie vijana kabla ya kupost wapitie maelezo na picha mara mbilimbili. Hii si mara ya kwanza kuwa na picha isiyoendana na maelezo.
ReplyDeleteMdau,
Mashariki ya Mbali.