Waziri wa Wizara ya Ujenzi  Dkt. John Pombe Magufuli, akisisitiza jambo wakati wa kufunga Mkutano wa Makandarasi uliofanyika leo Mlimani City.kulia  ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. John Ndunguru.
Wakandarasi na wahandisi, Ally Deffu(kulia) na Sadik Msangi, baada ya kupokea vyeti kwenye Mkutano wa Makandarasi wa Miaka 50 baada ya Uhuru.

Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Pombe Maghufuli, akiwasili kufunga Mkutano wa makandarasi wa miaka 50 baada ya Uhuru, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City leo,jijini Dar Es Salaam.

Mgeni Rasmi kwenye Sherehe ya Makandarasi na Wandisi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Dkt. John Ndunguru, akifungua Rasmi sherehe iliyofanyika kwenye viwanja vya Mlimani City leo jijini Dar.  Picha na Shaaban Mpalule

SERIKALI imehaidi kutoa kipaumbele kwa wakandarasi, wahandisi na wasanifu majengo wazalendo ili waweze kupata zabuni za ujenzi ya miradi mikubwa ambayo itaweza wajengea uwezo wa kujitangaza ndani na nje ya nchi.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilali wakati wa kufunga mkutano wa wadau wa sekta ya ujenzi uliomalizika jana.Dk Magufuli alisema kuwa, sezabuni za ujenzi zitakazoweza kujitangaza, kutokana na hali hiyo wamewataka wadau hao kuhakikisha kuwa, wanatumia nafasi hiyo ili waweze kujiongezea ufanisi mkubwa.

Alisema, kutokana na hali hiyo wadau hao wanapaswa kuhakikisha kuwa., miradi wanayojenga inakidhi kiwango kinachokubalika ili waweze kupata soko la ndani na nje ya nchi ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuitangaza nchi kwa ujumla.

"Ninachotaka kuwaambia ni kwamba, mnapaswa kuwa makini pindi mnapokuwa kwenye miradi, hii itaweza kuwatangaza na kuwatafutia masoko ndani na nje ya nchi, kutokana na hali hiyo mnatakiwa kutengeneza miradi inakidhi kiwango katika wakati uliopangwa,"Alisema.

Aliongeza, tabia ya baadhi ya watu ya kuomba rushwa katika miradi hiyo ni mbaya,inarudisha nyuma utendaji wa kazi zenu, na kwamba mnashindwa kuwa makini pindi mnapokubaliwa kwenye zabuni za ujenzi kwa sababu mmepoteza sifa ya kupewa zabuni hiyo.

Alisema, kutokana na hali hiyo mnapaswa kubadilika na kujiamini katika kazi zenu ili muweze kuaminika zaidi kwa wadau mbalimbali na si serikali peke yake.Alibainisha kuwa, kwa sasa serikali inatambua tatizolinalowakabili  la ukosefu wa mitaji, kutokana na hali hiyo wameziomba taasisi za fedha kuwakopesha ili muweze kununua vifaa ambavyo vitawasaidia katika kazi zenu.

Hata hivyo, serikali imehaidi kuwalipa deni lao la  Sh320bilioni lililotokana na mikabata mbalimbali ya ujenzi ambapo kwa sasa wako kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa, deni hilo linalipwa kwa wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...