Ubalozi wetu wa Tanzania Hapa Nchini Uingereza Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wamewateua Linda Kapinga na Lucy Minde ili kwenda kutuwakilisha katika mkutano wa nne wa Commonwealth Youth Parliament ( Bunge la Vijana) ulioanza tarehe 6-10 Septemba 2011 jijini London.
Kushoto Lucy na Linda katika picha ya pamoja Ubalozini.
Mkutano huu Umeandaliwa na Commonwealth Parliamentary Association tawi la Uingereza ikishirikishwa na Sekretarieti ya CPA ambayo ni Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Katibu wake ni Mwafrika wa kwanza kuteuliwa na Pia ni Mtanzania mwenzetu Dr William Shija.
Mh Naibu Balozi katika picha ya pamoja Lucy na Linda walioteuliwa kutuwakilisha katika Bunge la vijana.
Mh. Naibu balozi kwenye picha ya Pamoja akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi, TMK na mapromota wao waliokuja kuwaunga mkono Lindon.
Lucy Akitoa Ufafanuzi wakati wa mahojiano.

Urban Pulse Na Miss Jestina wakifanya mahojiano na Linda.
Lengo kuu la mkutano huu ni kuwawezesha vijana kati ya miaka 19-29 kwa kuwapatia uzoefu wa shughuli za Bunge hasa katika kuimarisha demokrasia ya mabunge na Uchumi. Motto wa Mkutano wa mwaka huu "MABADILIKO YA HALI YA HEWA"

Ubalozi wa Tanzania hapa Uingereza unapenda kuwapongeza sana Linda Kapinga na Lucy Minde kwa kuchaguliwa kwao na pia kuwatakia kila la kheri katika kutuwakilisha kwenye mkutano huu.

Asanteni,
Hisani ya Urban Pulse ikishirikiana Miss Jestina Blog Na Ubalozi wa Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. as far as I know hiy sehemu ilowekwa tv ni sehemu ya moto sasa sijui baridi ikifika itakuaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...