Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla walipokea kwa masikitiko, huzuni na majonzi makubwa taarifa ya kuzama kwa Meli ya MV.Spice Islander katika Bahari ya Hindi karibu na Nungwi usiku wa kuamkia tarehe 10 Septemba 2011 ambapo watu 612 waliokolewa wakiwa hai na maiti 203 zimepatikana mpaka sasa. Ili kujua ukweli kuhusu chanzo cha ajali hiyo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuunda Tume ya kuchunguza ajali hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee inaeleza kwamba kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi Sura ya 33 ya Sheria za Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ameunda Tume ya Kuchunguza Ajali ya Kuzama kwa Meli ya MV. Spice Islander ambayo itakuwa na Mwenyekiti, Wajumbe na Katibu kama ifuatavyo :-
Mwenyekiti wa Tume hiyo , Mhe. Jaji Abdulhakim Ameir Issa ni Mwanasheria mzoefu ambae kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Meja Jenerali S. S. Omari ni Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),COMDR. Hassan Mussa Mzee ni Mkuu wa Kikosi cha KMKM na Capt. Abdulla Yussuf Jumbe ni Nahodha mzoefu wa meli za kitaifa na meli za Kimataifa, ambapo pia aliwahi kuwa nahodha wa Meli ya MV. Mapinduzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Capt. Abdulla Juma Abdulla, alikuwa katika Kikosi cha KMKM kwa muda mrefu ambapo sasa ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Idara Maalum za SMZ na Bw. Salum Toufiq Ali ni Mwanasheria wa siku nyingi Zanzibar ambae ana uzoefu wa sheria za bahari, ambae kwa sasa ni Mwanasheria wa kampuni ya ZANTEL.
Capt. Hatibu Katandula ni Mkufunzi katika chuo cha Ubaharia cha Dar es Salaam na Bi Mkakili Fauster Ngowi ni Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Tanzania.
Bw. Ali Omar Chengo aliwahi kuwa mwanajeshi katika JWTZ na baadae kufanya kazi kwa muda mrefu katika Kikosi cha KMKM kabla ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na Naibu waziri wa Mawasiliano katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huko nyuma.
Katibu wa Tume hiyo Bw. Shaaban Ramadhan Abdulla ni mtaalamu wa Sheria za bahari, ambapo kwa sasa ni Mwanasheria katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP).

- Mhe. Jaji Abdulhakim Ameir Issa – Mwenyekiti
- Meja Jenerali S.S Omari – Mjumbe
- COMDR. Hassan Mussa Mzee – Mjumbe
- Capt. Abdulla Yussuf Jumbe – Mjumbe
- Capt. Abdulla Juma Abdulla – Mjumbe
- Bw. Salum Toufiq Ali – Mjumbe
- Capt. Hatib Katandula – Mjumbe
- Bi. Mkakili Fauster Ngowi – Mjumbe
- Bw. Ali Omar Chengo – Mjumbe
- Bw. Shaaban Ramadhan Abdulla - Katibu
Mwenyekiti wa Tume hiyo , Mhe. Jaji Abdulhakim Ameir Issa ni Mwanasheria mzoefu ambae kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Meja Jenerali S. S. Omari ni Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),COMDR. Hassan Mussa Mzee ni Mkuu wa Kikosi cha KMKM na Capt. Abdulla Yussuf Jumbe ni Nahodha mzoefu wa meli za kitaifa na meli za Kimataifa, ambapo pia aliwahi kuwa nahodha wa Meli ya MV. Mapinduzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Capt. Abdulla Juma Abdulla, alikuwa katika Kikosi cha KMKM kwa muda mrefu ambapo sasa ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Idara Maalum za SMZ na Bw. Salum Toufiq Ali ni Mwanasheria wa siku nyingi Zanzibar ambae ana uzoefu wa sheria za bahari, ambae kwa sasa ni Mwanasheria wa kampuni ya ZANTEL.
Capt. Hatibu Katandula ni Mkufunzi katika chuo cha Ubaharia cha Dar es Salaam na Bi Mkakili Fauster Ngowi ni Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Tanzania.
Bw. Ali Omar Chengo aliwahi kuwa mwanajeshi katika JWTZ na baadae kufanya kazi kwa muda mrefu katika Kikosi cha KMKM kabla ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na Naibu waziri wa Mawasiliano katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huko nyuma.
Katibu wa Tume hiyo Bw. Shaaban Ramadhan Abdulla ni mtaalamu wa Sheria za bahari, ambapo kwa sasa ni Mwanasheria katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP).
Mustafa Aboud Jumbe ndiyo mkurugenzi wa Bandari Zanzibar, na kaka yake (cousin) Abdulla Yusuf Jumbe ni mmoja wa wajumbe wa hiyo kamati.
ReplyDeleteJee hapo imekaa sawa?
Hii Kamati mimi nahisi haitokuja na jibu lolote,kwanza hilo jopo nahisi halina utaalamu na uelewa (expertriate) wa kutafuta kwa kina chanzo cha ajali.
ReplyDeleteKama mdau alivosema hapo juu kwa kuanzia tu Abdalla Jumbe na Yussuf Jumbe tayari kuna conlict of interest, na hapa naona mwanamke ni mmoja tu, wanawake wana uchungu wa uzazi kwa vile watoto wengi walikufa nilitegemea kuona timu sawa ya wanawake. Hapo naona hakuna Naval Engineer wala hakuna Naval Architecture.
Anyway haya kamati imeshaundwa, basi tunaomba mambo ya udugunizesheni (nepotism) uwekwe kando na haki za marehemu zizingatiwe, tafadhali tunaomba itendeke haki na sheria juu ya roho za walalahoi wasio na mtetetezi.
Tume ya nini? Melli ilikuwa na watu 3000 wakati inatakiwa watu chini ya 500. Sheria ziangaliwe na kufuatwa. Tume ni ulaji tu haitakuja na chochote kipya tusichokijua.
ReplyDelete