Pili ni pale kaka Ndesanjo Macha aliponitahadharisha kwamba ukianza kublog ni sawa na kujiambukiza ugonjwa usiotibika. Yaani mtu unakuwa kama umeehuka na hufikilii jambo linguine zaidi ya kublog. Macho kumchuzi yakaja tena. Ilikuwa ngumu kumuamini kwamba haka ‘kaugonjwa ka kublog’ kakikuingia mwilini hakatoki. Sasa naamini maneno yake maana haipiti dakika bila kuwaza niwatumikie vipi wadau.
Tatu ni pale kaka Ndensanjo Macha aliponitahadharisha kuhusu comment moderation. Yaani hii ya kupitia maoni yote yanayotumwa na kuchuja yanayofaa kusomeka na yasiyofaa, kwa mujibu wa sera za blogu yako. Macho kumchuzi yakaja tena. Safari hii ni kwa sababu wakati huo sikuwahi kuwaza kwamba kuna wadau ambao kazi yao ni kutukana, kujeruhi hisia za watu na kuchafua hali ya hewa. Hakika sikuwa nimemuelewa hadi baada ya kuanza kupitia maoni takriban 3000 kwa siku. Nashukuru kwamba kazi hiyo, yenye lawama tele kutokana na baadhi ya wadau wachache kutaka kutema cheche zao kupitia Globu ya Jamii kujikuta wakikwama, wakisahau kwamba sera ya Globu ya Jamii iliyotanabaishwa kila unapotaka kutuma maoni ya 'Angalia usijeruhi hisia za mtu/watu' inabakia pale pale kwa nia njema hiyo hiyo, na si vinginevyo.
Mtu mwingine aliyenitia hamasa kuendeleza libeneka baada ya kuanzisha blog ni kaka yangu, rafiki yangu na mpiganaji mwenzangu, Fidelis Tungaraza, aka Mti Mkubwa, aka FIDE. Huyu bwana, ambaye anaishi Helsinki, finland, kwa miaka kibao sasa, alikuwa daima akinicharuta mimi na waandishi wenzangu kuwa hatuwatendei haki wadau wa ughaibuni, kwani habari na taswira za nyumbani walikuwa wanazipata kiduchu mno kiasi kwamba ilikuwa sawa na kusema hakuna.

Baada ya hapo, na kama wanavyosema wahenga wetu, kila kitu ni historia. Niliporejea Tanzania nikaanza kufuata maelekezo ya Fide, kwamba niachane na mikutano, makongamano, warsha na mengineyo, bali niwaletee mambo ya jamii. Na ni yeye Fide aliyenipa majina ya Globu ya Jamii na wadau.
Mwaka mmoja baadaye, yaani mwaka 2006, nikiwa jijini New york, nikapata barua pepe toka kwa muasisi wa Globu ya Jamii, kaka Ndesanjo Macha. Akanipa pongezi na pole kwa kuendelea kuteseka na ugonjwa wa Ku-blogu. Pia akanikumubusha kwamba comment moderation nisiache hata siku moja, kwani SERA ya blog inaimarisha blog husika kwa kuzingatia hayo.
Mambo kadhaa yalijiri kuitambulisha Michuzi Blog kwa jamii baada ya hapo. Na mambo hayo yote yaliibuka chini ya kichwa cha habari cha BREKING NYUUUUZZZZZZ……ambapo kila mara hii ilimaanisha kwamba habari na taswira hizi ni za kipekee, za sasa hivi na hakuna ambaye anazo zaidi yangu mimi.
Nachelea kutaja BREKING NYUUUZZZ ZZ zote kwa uhaba wa nafasi, lakini zile za kuuwawa kwa wapendwa wetu Marekani (Nkya na Mazula), Kifo cha Mh Amina Chifupa na kujiuzuru kwa Waziri mkuu Mh Lowassa pamoja na kutajwa kwa baraza jipya la mawaziri ni baadhi tu ya habari moto ambazo Globu ya Jamii iliweza kuwa ya kwanza kutangazia ulimwengu kabla ya mtu yeyote ama chombo kingine cha habari.

Kama nilivyosema awali, mengine yote ni historia. Itoshe tu kusema kwamba nitachukua muda mrefu kueleza kila kitu na nisiweze kueleza robo ya mambo yote. Kwa maelezo hayo naomba ruksa niishie hapa na kuwaomba wadau mbofye sehemu ya ‘KUMBUKUMBU’ na kurejea katika posti za nyuma na kuapata hisoria kamili ya Michuzi Blog. Kila kitu kipo hapo.
Mwisho naomba nisema kwamba Michuzi Blog aka Globu ya Jamii ni mtumishi wa wadau wote duniani. Haichagui wala haibagui, kwani atayetuzika hatumjui. Hivyo nawakaribisha wadau wote tusherehekee siku hii huku nikiwaambia kwamba wakati wa kutimiza miaka 10 (InshaAllah) kutakuwa na MichuziTV na MichuziRadio Online, ambazo ziko njiani hivi karibuni.

Natoa shukrani kwa mdau aliyetoa wazo la kubadili jina ili Libeneke liwe la kimataifa, huku nikimhakikishia kwamba kuwa kimataifa sio lazima lugha iwe tofauti na Kiswahili, kwani tayari watu takriban milioni 400 wanazungumza lugha yetu ya Taifa ambao ndio walengwa wakuu.
Ahsanteni sana wadau kwa sapoti yenu katika muda wote huu na InshaAllah Mola akipenda na panapo majaaliwa MichuziTV na MichuziRadio Online itaibuka hivi karibuni humu humu ndani ya Globu ya Jamii kukuletea mambo kwa sauti na taswira zinazotembea. Tuombeane uzima tu.
Ni vigumu kumshukuru kila mtu aliyechangia mafanikio madogo haya ya Globu ya Jamii. Ila kwa uchache niwashukuru washauri, wachangiaji, walezi pamoja na timu nzima ya Michuzi Blog kwa kufanikisha haya yote.
Nianzie kwa washauri wakuu ambao baadhi ni kama JK, kaka Jeff Msangi wa Bongo Celebrity, Profesa Mark Mwandosya na mama Lucy Mwandosya, Jacob Mwambegele, Freddy Macha, Da'Chemi Chemponda, Balozi Juma Mwapachu, Balozi Peter Kallaghe, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, Da' Maura Mwingira, kaka Charles Hilary, kaka Abubakar Liongo, kaka Abou Faraji, kaka Ayoub Mzee, Da' Flora Nducha, kaka Freddy Maro, Dr Emmanuel Nchimbi, kaka Hilary Bujiku, Mh Zitto Kabwe, Mh. January Makamba, Mh John Mnyika, kaka Max Melo, Dr Prosper Mosha, Dr Blandina Kilama, Bi Ainde Ndanshau, Da' Teddy Mapunda, kaka Baraka Msiilwa, kaka Frank Eyembe, Da' Sporah Njau, Da' Subi, Da' Jestina George, Da' Mishi Marshall, Kaka Imani Kajura, Da' June Warioba, kaka Assah Mwambene, kaka James Shang'a, Dr Ramadhani Dau, Dr Kashilila, Da' Suzan Mzee, Da'Mariam Mungula, kaka Beda Msimbe, Dr John Shoo, Sensei Rumaza na Sensei Malekia, kaka John Mashaka, Profesa John Mbele, Dr Hassan Mshinda, Da' Mindi Kasiga, Ras Makunja 'FFU', Da'Janeth Mtonyi, Mh Mohamed Dewji, kaka Azim Dewji, Da' Mwamvita Makamba, Da' Taggie Daisy Mwakawago, Kaka David Minja, kaka Ephraim Mafuru, kaka Wilna, Dr Faustine Ndugulile na wengineo kadhaa ambao ni wengi mno.
Pia niwashukuru wana Globu ya Jamii wakuu kina Christopher Makwaia 'MK', Francis Dande, Audax Mutiganzi, Woinde Shizza, Muhidin Amri, Othman na Ahmad Michuzi, John Nditi, Prosper Minja, David Owen, Dixon Busagaga, John Mashaka, Dr Hildebrad Shayo, Frank Kallaghe, Othman Mapara, Richard Mwaikenda, Fide Tungaraza, Maggid Mjengwa, Haki Ngowi, Gadna G Habash, Lady JD.
Nawashukuru sana sana sana kwa sapoti yenu. Mie sina cha kuwapa Ila Mola ndiye atayewazawadia kwa wema na ushirikiano wenu.

-MICHUZI
Ankal akipongezwa na Ndesanjo Macha mara baada ya kufungua Michuzi Blog katika ukumbi wa Finlandia hall jijini Helsinki, Sweden, Septemba 8, 2005.
Happy Birthday Blog Ya Jamii. vital tool for our linkage across the globe.
ReplyDeleteMungu Ibariki Tanzania
John Mashaka
Kaka Michuzi,
ReplyDeleteHakika ni Siku Kuu. Michuzi blog ni zaidi ya blogu. Ni sehemu yetu ya maisha. Unajua kaka, kuna tulio nyuma yako. Tunajifunza. HONGERA SANA!
Maggid,
Iringa.
Blog ilifunguliwa jijini helsinki finland na sio sweden kama ilivyoandikwa.Happy birthday
ReplyDeleteNichukue fursa hii kukupongezeni kwa Blogi yetu ya Jamii kutimiza miaka 6 toka kuhasisiwa kwake.
ReplyDeletePia, nikiwa mdau niliyeshauri maboresho ya jina la blogi yetu hapo juzi,nichukue nafasi hii kuwashukru wadau waliotoa maoni yao bila woga na kwa uwazi zaidi kwa mantiki ya kuiboresha blogi yetu hii ya jamii katika nyanja ya habari.
Mwisho,napenda kuwashauri wamiliki wa blogi nyingine ndani na nje ya nchi,waige mfano wa kaka Issa na blogi ya jamii kwa ujumla ili kufikia malengo yao na malengo ya jamii kama ilivyokusudiwa kupitia tasnia ya habari.
Mdau: Joachim Kulwa Junior.
India.