kwanza kabisa napenda kukusalimia Ankali Habari za muda huu, nikitumai ya kuwa wewe ni mzima wa afya njema, mimi pia nikiwa ni mzima kabisa huku nikiendelea kusukuma Gurudumu kama kawaida.
Baada ya hili napenda kuchukua nafasi hii ya kipekee kukupongeza kwa kazi nzito iliyo simama ya kuliendeleza libeneke la GLOBU ya jamii mpaka kufikia miaka sita bila kuteteleka, hii inaonesha ukomavu wa Hali ya juu katika hii fani maana naamini kuna ambao walianzisha libeneke kama wewe lakini yalikufa zamani sana.
Kutoka na na hili Ankali pia nimeguswa sana na nimeona nishiriki kwa njia moja ama nyengine kwa kukuandalia tukio maalum kabisa ambalo nimeliandaa binafsi linalo onesha safari yako ya kublog ilipo anza tangia mwaka 2005 mpaka kufikia Leo hii unatimiza miaka sita Hiyo hapo chini ni link maalum ambayo ipo kwa Youtube.
kumbu kumbu hii iwe maalum kabisa kwako , Mwisho binafsi napenda kukushukuru sana sana kwa kunisaidia katika libeneke la Mbeya yetu umekuwa ni msaada mkubwa Kwangu na paka ukaipa jina la Libeneke Dada la Globu ya Jamii.
sina maneno Mazuri sana ya kukushukuru wala kitu cha kukupa lakini nasema Asante sana na Mwenyezi Mungu azidi kukuzidishia pale palipo pungua paongezeke zaidi, Nikutakie Maisha mema na afya njema, Hongera kwa Timu Nzima ya Libeneke la Globu ya jamii.
Aluta kontinua mapambano yanaendelea Libeneke Hoyeeeeee!!!!!
Mwanalibeneke,
Fredy Tony.
Msimamizi mkuu Mbeya yetu Blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...