Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari na wadau mbalimbali kuhusu mwelekeo wa mvua za vuli za mwezi Oktoba – Desemba 2011 leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema maeneo mengi ya nchi yatapata mvua za wastani na juu ya wastani na kutoa tahadhari kwa wafugaji, wakulima, sekta ya afya na mamlaka za miji nchini kuzibua mitaro ili kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakifuatilia taarifa ya mwelekeo wa Hali ya hewa iliyotolewa na Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi(hayupo pichani) leo jijini Dare Salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Na. ESTHER MUZE - MAELEZO.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imesema mvua za vuli katika maeneo mbalimbali zinatarajia kuanza mwezi Oktoba huku maeneo ya kanda ya ziwa yakitarajia kupata mvua zaidi ya juu ya wastani.

Akizungumza na waandishi wa habari na wadau mbalimbali juu ya mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2011 leo jijini Dar es salaam, Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes Kijazi amesema mvua hizo zitasababisha upatikanaji wa maji nchini kuongezeka na kusababisha ongezeko dogo la kina cha maji katika mabwawa ya maji nchini.

Amesema katika maeneo ya kaskazini ya nchi mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi Septemba na kuendelea kusambaa katika maeneo mengine yanayopata mvua misimu miwili kwa mwaka hasa maeneo ya kanda ya Ziwa Victoria yakihusisha mikoa ya kagera , Mara, Mwanza, Shinyanga na kigoma kaskazini.

Ameongeza kuwa ukanda wa Pwani ya Kaskazini Mikoa ya pwani , Dar-es- Salaam, Tanga, Morogoro, kaskazini-mashariki , Visiwa Vya Unguja na Pemba mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya pili ya mwezi Oktoba ambapo maeneo ya nyanda za juu Kaskazini mashariki yanayohusisha mikoa ya Kilimanjaro , Arusha, na Manyara Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya tatu ya mwezi oktoba 2011 na kuwa za wastani hadi juu ya wastani.

Aidha ametoa tahadhari kwa mamlaka mbalimbali za miji zinazohusika na sekta ya afya kuchukua tahadhari kuytokana na kuwepo kwa uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko sanjari na uzibuaji wa mitaro inayopitisha maji machafu ili kuepuka mafuriko katika maeneo mbalimbali.

Kwa upande wa shughuli za kilimo na mifugo ametoa wito kwa wananchi kuzingatia ushauri wa maafisa ugani na mifugo walio katika maeneo yao ili wafaidike na mvua hizo.

Hata hivyo amesema kuwa upatikanaji wa maji na nishati kwa ajili ya mifugo wanyama pori na matumizi mengine katika shughuli za kiuchumi na kijamii yanatarajiwa kuwa wa kutosheleza katka maeneo mengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...