Wakuu wa nchi walihudhuria mkutano wa ulijadili jinsi ya kukabiliana na tatizo la njaa na ukame katika nchi za pembe ya Afrika.kutoka kushoto ni Rais Salva Kiir wa Sudan ya Kusini,Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi,Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyopo Nairobi Bi.Sahle Work Zewle, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia na Makmu wa Rais wa Kenya Mh. Steven Kalonzo Musyoka
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed jijini Nairobi kabla ya kuanza kwa mkutano uliojadili jinsi ya kukabiliana tatizo la njaa na ukame katika nchi za pembe ya Afrika.Katikati ni mwenyeji wa mkutano huo Rais Mwai Kibaki wa Kenya.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mwenyeji wakeRais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa siku moja uliojadili tatizo la njaa na ukame linazozikabili nchi za pembe ya Afrika uliofanyika katika kituo cha Umoja wa mataifa uliopo Gigiri, nje kidogo ya jiji la Nairobi,Kenya leo asubuhi. Rais amesharejea nchini. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...