Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bwana John Haule akiwa kwenye mazungumzo na mjumbe maalum kutoka Serikali ya Australia Bwana Leslie Rowe leo tarehe 12-9-2011. Bwana Rowe yuko nchini kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Madola unaotarajiwa kufanyika mjini Perth Australia mwishoni mwa mwezi ujao. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bibi Dora Msechu.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bwana John Haule akimkaribisha mjumbe maalum kutoka Serikali ya Australia Bwana Leslie Rowe wizarani leo aliyeko nchini kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Madola unaotarajiwa kufanyika mjini Perth Australia mwishoni mwa mwezi ujao.Picha na  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...