UMOJA WA WANAFUNZI WA KITANZANIA WASOMAO KATIKA CHUO KIKUU CHA URAFIKI (LUMUMBA) MJI WA MOSCOW NCHINI URUSI, UNAPENDA KUTOA SALAMU ZA POLE KWA WATANZANIA WENZAO KUFUATIA AJALI YA MELI ILIYOPINDUKA NA KUZAMA KATIKA VISIWA VYA ZANZIBAR MNAMO SIKU YA JUMAMOSI MAJIRA YA USIKU WA MANANE NA KUSABABISHA VIFO KADHAA VYA ABIRIA WALIOKUWEMO KATIKA MELI HIYO WAKIWA SAFARINI KUTOKA UNGUJA KUELEKEA PEMBA.
KWA PAMOJA TUNASEMA MSIBA HUU NI WETU SOTE NA TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AWALAZE MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI,AWAPE SUBIRA WAFIWA NA AWAPE SHIFAA NA TAHAFIFU MAJERUHI NA WOTE WALIONUSURIKA NA KADHIA HIYO.
KWAKE TUMETOKA NA KWAKE NI MAREJEO.
AMEEN!!!!!!
UONGOZI WA WANAFUNZI-UWATA
UONGOZI WA WANAFUNZI-UWATA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...