Magari Makubwa ya kubeba mizigo mizito yakiwa yamepaki katika Barabara ya Mandela Road kwa ajili ya kuingia kwenye yadi maalum iliyotenga na Mamlaka ya Bandari kwa ajili ya kuhifadhia makontena ya mizigo inayotoka bandarini iliopo Tabata AMI-ICT maeneo ya Relini jirani kabisa na Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya Mwananchi.hali hii imekuwa ni kero kubwa sana kwa watumiaji wa barabara hiyo na wakazi wa maeneo ya jirani na yadi hiyo,kwani kuna kipindi magari hayo yanalazimika kufunga kabisa barabara hiyo ya Mandela kutana uzembe wa madereva wa magari hayo kutaka kuingia kwenye yadi hiyo bila yafuata utartibu.huku tatizo lingine likidaiwa kuwa ni utaratibu mbovu uliopo ndani ya yadi hiyo ambao kwa namna moja au nyingine unachangia kuongeza kero hii ya haya mabari kupaki hovyo barabarani.
Kuna kipindi inafika hata hii njia nyingine inakuwa imefungwa kutoka na magari hayo makubwa kupaki bila ya mpangilio.
Sasa imehamia upande wa pili wa barabara,kule wamefunga njia zote hadi sevisi rodi.
Hiyo ni barabara ya magari amkubwa yatokayo bandarini waacheni wajinafasi.Ndiyo maana kabla ya kuitwa mandela road ilikuwa inaitwa port access.
ReplyDelete