Balozi wa Brazil nchini Mh. Francisco Luz akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya "AMRIK" yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Brazil, Taasisi za nchi za Kiarabu na Aga Khan. Ambapo Balozi huyo amewapongeza walioshiriki maonyesho hayo. Maonyesho hayo yenye lengo la kuhamasisha ushirikiano kati ya Wabrazil na Waarabu yalitarajiwa kufanyika wiki iliyopita lakini yakaahirishwa kufuatia ajali ya kuzama kwa Meli ya MV SPICE ISLANDER iliyotokea huko Zanzibar.Katikati ni Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu na Kushoto ni Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan Bw. Navroz Lakhani.
Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu akisoma hotuba kwa wageni waalikwa katika maonyesho ya Picha yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan Bw. Navroz Lakhani ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maonyesho hayo akizungumza machache katika hafla ya ufungaji wa maonyesho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...