Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la Bia Tanzania lijulikanalo kama ‘Kilimanjaro Beer Festival’ litakalofanyika katika viwanja vya Leaders club kwa siku mbili mfululizo kuanzia kesho kutwa. Pamoja naye ni wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma, Romario Mng’ande (kulia) na Said Mabera.
Mwimbaji na Kiongozi wa Bendi ya Akudo Impact, Ebolo Litumbi “Canal Top” akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Bia Tanzania ambalo linajulikana kama ‘Kilimanjaro Beer Festival’ litakalofanyika kwasiku mbili mfululizo kuanzia kesho kutwa katika viwanja vya Leaders club jijini Dar es Salaam. Kulia ni Madee na Patick Mbuyanzi wa Akudo Impact.
Baadhi ya wasanii mbalimbali wa muziki wa dansi na ule wa kizazi kipya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Bia Tanzania lijulikanalo kama Kilimanjaro Beer Festival litakalofanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia kesho kutwa katika viwanja vya Leaders club jijini Dar es Salaam.Nyuma kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe.

Wasanii zaidi ya kumi watakaotumbuiza katika Tamasha la kwanza la Bia Tanzania Jumamosi na Jumapili katika Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam wameahidi kutoa burudani ya aina yake kwa watanzania.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wasanii hao na wawakilishi waliishukuru Bia ya Kilimanjaro Premium Lager na Kampuni ya Bongo 5 kwa kuandaa tamasha hili kubwa la kwanza na la aina yake Mkoani Dar es salaam,  .

Baadhi ya wasanii na makundi yaliyohudhuria mkutano huo na waandishi wa habari ni Chidi Benz, Msondo Ngoma, Twanga Pepeta, Akudo Impact, Canal top, Tip Top, Ben Paul, Linex, Linah na THT ambao waliwapa wandishi wa habari vionjo kidogo ya vitu ambavyo watavifanya katika tamasha hili.

Kilimanjaro Premium Lager ikishirikiana na Kampuni ya Bongo 5 na Taasisi ya Goethe wanaandaa tamasha kubwa la bia la kwanza Tanzania ambalo litafanyika katika Viwanja vya Leaders Octoba 1 na 2 mwaka huu.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Bw. George Kavishe alisema tamasha hili litakalojulikana na Kilimanjaro Beer Festival, litakuwa la kwanza na la aina yake kuwahi kufanyika Dar es salam, Mwaka 2007 tuliandaa tamasha kama hili Mkoani Kilimanjaro na 2008 tulifanya Mkoani Arusha na yalikuwa na mafanikio makubwa, sasa tunafanya Dar es salaam  tukiwa na madhumuni ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru na kuwaleta Watanzania pamoja.

Alisema miongoni mwa waalikwa ni wasanii mbalimbali wa Bongo Movies ambao  watajichanganya na watu na kubadilishana mawazo nao na kucheza mechi ya kirafiki na timu zambalimbali za Veterani.

Tamasha hilo litaanza saa nne kamili asubuhi na litaendelea kwa siku mbili mfulululizo, hadi usiku na kwamba tiketi zitauzwa Tsh 10,000 kwa siku zote mbili na Tsh 7,000 kwa siku moja.

Bw. Kavishe aliwaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili waburudike na kujivunia mafanikio yao baada ya miaka 50 ya Uhuru.

Kwa upande wake, Mratibu wa Matukio, Olive Nimaga aliishukuru TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa jitihada zake za kuwatambua na kuwathamini wateja wake kwa kukukubali kudhamini tamasha hilo la aina yake.

“Tunawahakikishia mazingira mazuri na salama wakati wa tamasha hili kwani itakuwa wikiendi yenye burudani mbalimbali,” alisema.

Alisema baadhi ya wasanii watakaotoa burudani ni pamoja na Linah, Linex, Chidi Benz, Godzilla, Offside Trick, Akudo Impact, Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wengineo. “Kutakuwa na nyamachoma na vyakula vingine vya aina mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Master guitarist Said Mabera. A true Tanzanian legend.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...