Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kigoma vipi :-)??? Zitto, Kawambwa, namna gani pale? '...@yahoo,com', I really don't 'no' what to say anymore but this is very disappointing and shameful. Hata hiyo 'NABADO' nayo haiko sawa, ilipaswa iandikwe 'NA BADO.' Kumbe yasemwayo kuhusu Kigoma ni kweli kabisa. Kama hata maelezo ya airport yanachakachuliwa sembuse mitaani? For 'here' stopisha hia hia.

    ReplyDelete
  2. Kiingereza ovyo na kiswahili pia ovyo, si kigoma tu nchi nzima. Elimu imeshuka, tukubaliane. Walimu, wabunge, watangazaji asilimia kubwa hawawezi kujieleza kwa ufasaha kwa lugha hizi zetu sembuse za makabila.wajua ingewezekana watnzania kukifanya kiswahili kuwa bidhaa ya kutuingizia kipato cha ndani na nje kwa kufundisha lakini .....kwenye miti hakuna wajenzi kila mmoja anataka kufika peponi bila kufa|

    ReplyDelete
  3. Hivi hao wenye magari yao nao wanakuwa hawana hata kiingereza cha kuombea maji nini?

    ReplyDelete
  4. Hata raisi,wzr mkuu,wabunge na viongozi mbalimbali wanabananga sana kiswahili, baraza la kiswahili lisimamie lugha hii na kila anaekosea achukuliwe hatua, pia matangazo na vibao elekezi vyote viandikwe kiswahili, angalia mitaa,maduka, baa na saluni zilivyo na majina ya kigeni. KASUMBA. Kuna tatizo gani kuwa na Nyaminywili bar kuliko Goerge Bush Social Club pale Mbagala?

    ReplyDelete
  5. Kiingereza hata usome vipi kama hakuna mazoezi ya kusema basi ni taabu tupu. Lakini hili tatizo sio kwa waTZ tu bali hata watu wengine ambao tunafikiria wanasema kiingereza sana. Mfano Wanigeria na Wazambia hawa wanauzoefu wa kusema kiingereza hata kama shule amemaliza elimu ya msingi. Lakini ukimpa mtihani wa "english proficiency" hana tafauti na mTZ kwenye matokeo na pengine mTZ atapata matokeo mazuri. Pia kama utasoma blog za Wakerewe wenyewe basi grammar na spelling ni tatizo sugu! Kwa ufupi hata kiswahili pia watu kinatupa taabu. Kama kuna mtu anataka "contribution" ya PhD yake ya lugha basi hii blog ni safi sana maana makosa ya lugha ni mengi!!

    ReplyDelete
  6. Message sent ndio muhimu. Sio lazima mtu ajue kiingereza. Matajiri wengi wa Bongo hata kuweka sahihi ni taabu. Kina Mengi, Bakhresa, Manji hawakufika Chuo Kikuu. Kidogo Mengi anajitahidi kiingerez. Huu ndio unaitwa usanii mtu akiisoma anajiiuliza hivi amemaanisha nini huyu, halafu inamsumbua akilini, kama hivi tunavyosumbuka sisi halafu mtu akigongwa na hilo lorry ni rahisi kulipata. Nyie wadanganyika, ndizi mnakula nyingi lakini "'gray' meter do not boil". Mwandishi mwandamizi Maggid Mjengwa katika pata ya 5 ya makala yake ya kutetea Chadema ameandika neno 'alikadhalika', je amemaanisha nini. Ndio watu wanafeli somo la Kiswahili FOrm IV 'h' iko silent katika kilugha chao. Hahahahahaha.

    ReplyDelete
  7. Tatizo la watu wengi ni kuandika, analitamka neno lakini kuliandika ni shida tupu, na hasa haya maneno yanayofanana matamshi.

    ReplyDelete
  8. Wajameni ni nini sasa mbona mmeisha anzisha issue tena ya kigoma?

    Tuachani tule dagaa zetu bana mnatunyanyasa huyo rais wetu nae mbona

    kimombo hakipandi?

    ReplyDelete
  9. hiyo NABADO ingebidi waiweke kizungu kabisa "AND NOT YET"....like our old secondary school days

    ReplyDelete
  10. Ni nyie tu ndio mbumbu,hii yaweza ikawa ni mbinu ya kuvuta hisia zenu tu na wala si kwamba hao walioandika hawajui.

    ReplyDelete
  11. Tatizo liko kwa mwenye mali. Nyie hamwajui watani wangu wa jadi waha, ni wabishi kama nini! Kesha ambiwa arekebishe lakini amekataa. Lakini mimi nadhani si neno, ilimradi anayesoma anaelewa kile kinachomaanishwa. Mara nyingi tu hata mimi ninayejidhania kwa umbumbumbu wangu kuwa ni msomi nimefanya makosa ya kiufundi kama hayo katika uandishi wangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...