Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete akiwapa nasaha vijana wa UVIKIUTA katika kituo chao huko Mbagala Charambe,Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam leo alipowatembelea.kushoto ni Mwenyekiti wa UVIKIUTA, Ben Mongi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete akipatiwa maelezo na Mwenyekiti wa UVIKIUTA, Ben Mongi wakati alipotembelea katika kituo hicho kilichopo huko Mbagala Charambe.
Baadhi ya vijana wa taasisi ya maendeleo ya vijana nchini wakisikiliza nasaha kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) alipotembelea na kuona shughuli za taasisi huko Mbagala wilaya ya Temeke. UVIKIUTA lengo lake ni kuwajengea uwezo vijana katika maeneo mbalimbali ya kijamii na kuwawezesha kumudu maisha yao.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete akionyeshwa miche ya miti mbalimbali na Mwenyekiti wa Taasisi ya maendeleo ya vijana (UVIKIUTA) Ben Mongi (shati la kitenge) alipotembelea na kuangalia shughuli mbalimbali za taasisi huko Mbagala Mkoani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na vijana wa Taasisi ya maendeleo ya vijana (UVIKIUTA) mara baada ya kukutana nao na kuzungumza nao huko Mbagala,mkoani Dar es Salaam.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.


Honera sana UVIKIUTA, mwanzo ulikuwa mgumu sasa mafanikio yanaonekana. UVIKIUTA ni mfano wa kuigwa na vijana, Hongera Ben na wote walioshiriki kuanzisha na kuendeleza UVIKIUTA. Doro.
ReplyDeletehongereni ndugu zanguni wa UVIKIUTA. Nawatakia mafanikio zaidi na naamini matokeo mazuri kwa lolote mfanyalo.Big Up! wandugu
ReplyDelete