Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, Alferd Luanda,akisalimiana na Mkuu mpya wa Mkoa huo, Joel Bendera alipowasili Septemba 19, mwaka huu kwenye majengo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kukabidhiwa rasmi kazi ya kuwahudumia wananchi wake baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, Francis Miti , akisalimiana na Mkuu mpya wa Mkoa huo, Joel Bendera alipowasili Septemba 19, mwaka huu kwenye majengo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kukabidhiwa rasmi kazi ya kuwahudumia wananchi wake baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera , akisaini kitabu cha wageni kilichopo katika ofisi yake mpya mara alipowasili Septemba 19, mwaka huu kuanza rasmi kazi ya kuwahudumia wananchi baada ya kuteuliwa wadhifa huo na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni ( kulia) ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya,ambaye amehamishiwa Mkoa wa Kigoma.
Baadhi ya wafanyakazi wa serikali wa ngazi mbalimbali kutoka Wilaya za Mkoa wa Morogoro sambamba na wa Ofisi hiyo ya Mkoa wamejipanga kwa ajili ya kumkaribisha na kusalimiana na Mkuu mpya wa Mkoa huo, Joel Bendera, alipowasili Septemba 19, mwaka huu ili kukabidhiwa rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Issa Machibya ambaye amehamishiwa Mkoa wa Kigoma baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo.Picha zote na John Nditi.
Huyu Mh Joel Bendera alishawahi kuwa kwenye Wizara ya Mifugo?
ReplyDeleteahsante sana ankal kwa fursa hii adhimu,kwanza namongeza mh joel bendera kwa kuteuliwa kuwa rc moro,pili kwa mh raisi jk kuona kuwa mh bendera ni mtu muafaka kwa moro,mi si mkazi wa moro ila kwa rekodi ya mh bendera anastahili kupewa moro hasa kwa ishu ya soka.natarajia atatuvumbulia vipaji kama vya kina mogella(golden boy) hamisi gaga(gagarino),malota(balljuggler),na wengineo hao wa simba wanatosha,kwa kweli nategemea ule ususmbufu wa kukosa ma straika tanzania hueanda likapata ufumbuzi,
ReplyDeletepls zifikishe salaam na matumaini yetu kwake mh j bendera
abu man
mdau libeneke kigamboni