Na Audax Mutiganzi,Bukoba
MKUU mpya wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabian Massawe ameahidi kuendeleza mikakati yake ya kupambana na vitendo vinavyohatarisha amani ndani ya jamii ambayo aliibuni alipokuwa mkuu wa wilaya ya Karagwe.
Massawe alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipofanya mahojiano maalumu na ripota wa Globu hii ya Jamii kwa njia ya simu.
Mkuu huyo wa mkoa alisema atahakikisha anapambana na mafataki wanaowabebesha watoto wa shule mimba, alisema kuwa atahakikisha anawashughulikia wanaojihusisha na biashara ya magendo ya kahawa, pia alisema atahakikisha suala la usafi wa mazingira linazingatiwa.
Alisema alipokuwa mkuu wa wilaya ya Karagwe mikakati yake kwa asilimia kubwa ilifanikiwa kwa kuwa mafataki waliacha tabia ya kutembea na wanafunzi wa shule, aliendelea kusema magendo ya kahawa ilikoma na kila mwananchi alikuwa anahakikisha eneo lake linakuwa safi.
Massawe alisema pia atahakikisha kila mwanafunzi ambaye anafaulu mtihani wake wa elimu ya msingi anajiunga na kidato cha kwanza, alisema atawashughulikia wazazi watakaowaficha watoto ili wasiendelee na masomo.
Alisema mkoa wa kagera anaufahamu sana hivyo hautampa shida kubwa kuutembelea na kubaini matatizo yanayowakabili wananchi, aliendelea kusema yeye anachokitaka ni watu kufanya kazi kwa bidii ili waondokane na umaskini wa kipato.
Mkuu huyo wa mkoa alisema atahakikisha anawashughulikia wale wote wanaojihusisha na vitendo vya ulevi hasa wakati wa muda wa kazi, alisema vitendo vya ulevi vinachangia sana uvunjifu wa amani ndani ya jamii.
Aliwaomba wana Kagera wampe ushirikiano mzuri ili aweze kufanya kazi kwa urahisi zaidi, alisema wananchi wakimpa ushirikiano itakuwa rahisi kwake kutatua kero zinazowakabili wananchi.
Yeye binafsi aliahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi na kwa wale wasaidizi wake, pia aliahidi kushirikiana kwa ukaribu na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini.
Huyo alifaa sana kupelekwa Mbeya, manake watu wa kule hawasikii kabisa!!!1
ReplyDeleteMbona viongozi wa Kagera kila mara ni wanajeshi? Akitoka mmoja anaingia mwingine. Isipokuwa Babu ndiye alikuwa amevunja mfumo. Ni ajali au makusudi?
ReplyDeleteSimkoa hupo mpakani lazima usimamiwe na mtu mwenye akili za kijeshijeshi alafu si unajua Mtemi m7 yupo karibu pia hapo. uwezi mkabize mkoa huo kwa lelemama
ReplyDeleteMassawe alipokua karagwe alipambana sana na watu ambao hawafati sheria sijue atasaidi hivyohivyo mkoa wetu wa kagera
ReplyDelete