Ndugu zangu Watanzania nawaomba tumsaidie mtoto Halima Kassimu (12) pichani wa Nanenane Morogoro kwani mateso anayoyapata ni makubwa sana. Halima alizaliwa akiwa ni mlemavu wa miguu yote miwili na hakuweza kutembea (Kiwete). Wazazi wake walijaribu kumpeleka katika hospitali mbalimbali bila mafanikio. Mwisho wakiwa katika kukata tamaa wakaambiwa kuwa mtoto huyu anaweza kupona kama atapelekwa KCMC au CCBRT.

uvimbe kiunoni ambalo linamfanya asiweze kuhisi chochote kuanzia kiunoni hadi miguuni kiasi ambacho hata haja kubwa na ndogo zinatoka bila mwenyewe kujitambua. Alipofikisha miaka mitatu alitoka vidonda miguuni na havikupona mpaka alipofika miaka kumi na moja (2010) mwaka huu tena vimeanza kumtokea vidonda miguuni.
  Kutokana na kutokuwa na uwezo basi wazazi waliamua kumpeleka shule ya kawaida akiwa na watoto wenzake wasio na ulemavu. Yeye na pacha wake (Ismail) walikuwa darasa moja  lakini shule alimudu kusoma kwa miezi miwili tu. Walimu walimshauri mzazi wake amwachishe shule kwa kile walichosema anawachefua wenzie. Pacha wake yupo darasa la tano na Halima bado yupo nyumbani bila kujua hatima yake ya baadaye. Kwa hivi sasa Halima anaishi na mama yake na babu yake kwani baba yake amemtelekeza na anaishi na mtoto wa kiume ambaye ni pacha wa Halima asiye na tatizo lolote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. POLE SANA HALIMA NA MWENYEZI MUNGU ATAKUAFU INSHALLAH.SASA MICHU MBONA HUJAWEKA HATA A/C AU NUMBER ZA SIMU ILI WASAMARIA WEMA WATAKAOJITOLEA KUMSAIDIA?NA PENGINE WENGINE WATAPENDA KWENDA KUMUONA NA KUJITOLEA MSAADA WOWOTE.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli huyu mtoto anahitaji msaada.

    Ila mbona umeelezea shida na mateso yake tu? Tungependa kufahamu gharama ya matibabu au aina ya msaada, na sehemu ya kupeleka hiyo misaada.

    Mdau

    Amsterdam

    ReplyDelete
  3. hakuna simu ya kuwasiliana nao?

    ReplyDelete
  4. sasa msada gani unatakikana mbona hukutueleza na wapi upelekwe bebu tufafanuwa tukufahamu

    Abdullrasull

    Zanzibar

    ReplyDelete
  5. Mmmmh wanaume Mungu awasamehe kumuachia mama mzigo na kukimbilia nyumba ndogo ni dhambi kubwa na huyu mtoto mzuri hivyo ukaondoka na huko uliko ukipata mwenye matatizo zaidi utaondoka tena? Ok pole mdogo wangu, naamini Mungu wa mbinguni anakila sababu ya kukuumba hivyo na anawezo wa kukufanyia njia iwe kwa madaktari(hospitalini) au kwa kuombewa na kusaidiwa kama hivi. Nimesikia uchungu sana wa huyu bb kumwacha mke anayekusaidia kulea mtoto mwenye matatizo hadi kufikia umri huu. Sijui kwa kuwa mi ni pacha kama yeye? Anyway hili tangazo ni bubu maana yake hatujaambiwa tumsaidieje, hasa kama atakuja moshi wengine tungeweza kumsaidia hata vitu vidogo, vidogo kama nguo, chakula hela za matumizi. Please michuzi usikae kimya toa taarifa zote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...