Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamid Abdulkarim akiwa amemshika mkono Cesilia Edward (14) mwenye tatizo la moyo linalosababisha kuvimba tumbo akitoka Hospitali ya Regency jana tayari kwa safari ya New Delhi, India kwa matibabu.

Mtoto Cecilia Edward ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kuvimba kwa tumbo amewashukuru kwa moyo mkunjufu watanzania waliojitokeza katika kumsaidia kwa hali na mali mpaka kufanikiwa kupata hela tayari kwa matibabu anayotarajia kwenda kuyapata nchini India.

Cecilia amesafiri kuelekea katika hospitali iitwayo Fortis inayopatikana New Delhi -India kwa matibabu, jumatatu ya tarehe 26 mwezi septemba mwaka huu.

Aidha walezi wa Sesilia familia ya mzee Kambaliko inatoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliojitolea kwa moyo kumsaidia binti yao kwa kutoa pesa, mavazi na hata waliowapa maneno ya faraja pamoja na wale wote wanaoikumbuka familia hiyo katika maombi.

Kabla ya safari yake hiyo, hali ya kiafya ya sesilia ilikuwa ikiendelea vizuri, kwani alikuwa anaweza kupumua na kukaa, tofauti na awali kutokana na kupunguzwa kwa kiasi cha maji katika tumbo lake hospitalini Regency alipolazwa kwa ajili ya matayarisho kabla ya kuanza safari yake kuelekea nchini India kwa matibabu zaidi.

Mtoto huyu aliondoka hapa nchini jumatatu ya tarehe 26 na ndege ya shirika la Quatar Airways akifuatana na daktari mmoja kutoka hospitali ya regency, pamoja na mlezi mmoja mpaka nchini India alipotarajia kupokelewa na madaktari tayari kwa uchunguzi wa kina na kisha kuanza matibabu yake.

Kipindi cha Mimi na Tanzania kinapenda kuwashukuru Watanzania wote pamoja na makampuni mbalimbali yaliyojitolea katika kumsaidia Sesilia kwa ajili ya matibabu. Shukrani za pekee ziifikie hospitali ya regency hasa daktari Kanabar kwa uvumilivu na huduma nzuri kwa Sesilia. Pia kwa mchango wao wa kulipia nauli ya kwenda nchini India kwa Sesilia, mzazi na daktari ikiwa ni pamoja na matibabu ya awali anayoyapata hivi sasa.

Watanzania, pamoja tumeweza tena. Sesilia ni mmoja tu kati ya watoto milioni moja wanaosumbuliwa na tatizo hili, hebu tujitolee kuwasaidia watoto hawa bila ya kuchoka, pia tusimsahau binti huyu kwa maombi ili upasuaji anaotarajia kufanyiwa umalizike salama na kwa mapenzi yake Mungu mtoto huyu arudie katika hali ya kawaida kama watoto wengine.

Mungu mbariki Sesilia.Amen!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. ongereni sana wamiliki wa channel 10 , mmetoa mfano boro wa kuingwa na watanzani wengine.
    mdau pari

    ReplyDelete
  2. Ee Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema tunakuomba kwa umoja wetu watanzania uwawezeshe madaktari India watakaomshughulikia mtoto wetu Cecilia kufanya kazi hiyo wakiongozwa na wewe Mponyaji mkuu, mpe Cecilia uwezo wa kukabiliana na matibabu yote na mwisho wa siku apone na kurudia tena hali yake Amin!Ee Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema tunakuomba kwa umoja wetu watanzania uwawezeshe madaktari India watakaomshughulikia mtoto wetu Cecilia kufanya kazi hiyo wakiongozwa na wewe Mponyaji mkuu, mpe Cecilia uwezo wa kukabiliana na matibabu yote na mwisho wa siku apone na kurudia tena hali yake Amin!

    ReplyDelete
  3. Mungu atakusaidia upone Cecilia urudi uendelee na shule kama wenzako.

    Ukiwa mkubwa usomee udaktari.

    Channel 10 hongereni sana kwa juhudi zenu.

    ReplyDelete
  4. mwenyezi mungu atakuponya cecilia, amen.

    ReplyDelete
  5. Ee Mwenyezi Mungu muone mtoto wako anavyoteseka mpe amani moyoni, wape hekima na ufahamu, wape huruma ya hali ya juu madaktari wote watakaoenda kumfanyia oparation hiyo mtoto cecilia. Tunakutegemea wewe kwani wewe ndiwe bwana na mwokozi wetu. Amen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...