Kocha Mkuu wa Taifa Stars, 
Jan Poulsen
Kocha Mkuu wa Taifa Stars,Jan Poulsen leo  ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Morocco.

Kikosi hicho kitaingia kambini Septemba 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na kinatarajiwa kuondoka nchini Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Oktoba 9 mwaka huu kwenye mji wa Marrakech.

Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba). Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).

Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) na Jabir Aziz (Azam). Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Ramadhan Chombo (Azam).

Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...