Washiriki wakimsikiliza kwa umakini kabisa mtoa mada (hayupo pichani) juu ya ujuzi wa kuokoa maisha ya mama na mtoto
<
alt="DSC03685.JPG" height="480" src="https://mail.google.com/mail/?
ui=2&ik=6b212f65cf&view=att&th=1329638e2589b464&attid=0.5&disp=emb&zw"
width="640" />
Aliyesimama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
akitoa nasaha zake kwa wahitimu wa mafunzo.Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Idara
ya Magonjwa ya Akina Mama Dkt. Mathew Kalanga.
akitoa nasaha zake kwa wahitimu wa mafunzo.Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Idara
ya Magonjwa ya Akina Mama Dkt. Mathew Kalanga.
Aliyevaa sare ya Wauguzi ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za
Uuguzi Sr. Salome Mayenga akifuatiwa na Meneja wa Jengo la Wazazi Sr. Amina
Mwakuluzo akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujuzi wa kuokoa maisha
ya mama na mtoto
Uuguzi Sr. Salome Mayenga akifuatiwa na Meneja wa Jengo la Wazazi Sr. Amina
Mwakuluzo akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujuzi wa kuokoa maisha
ya mama na mtoto
Washiriki wa mafunzo ya kuokoa maisha ya mama na mtoto wakiwa katika picha ya pamoja
Hili ndo jengo la wazazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili
Wakati Rais Jakaya Kikwete akiwa amepokea tuzo mbili maalumu kutokana na mchango wake mkubwa katika afya ya mama na mtoto Jijini New York, leo zaidi ya wataalamu 60 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamehitimu mafunzo ya ujuzi wa kuokoa maisha ya mama na mtoto (life saving skills) iliyofanyika Hospitalini hapa.
Mafunzo hayo yalihusu mbinu mbalimbali za kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo si vya lazima vinavyotokana na kutokwa damu nyingi kabla, wakati na baada ya mama kujifungua, maambukizi katika mfumo wa uzazi, kifafa cha mimba, uzazi pingamizi na utoaji mimba usio salama, upungufu wa damu wakati wa uja uzito, maralia wakati wa uja uzito na upungufu wa kinga mwilini unaotokana na maambukizi ya UKIMWI.
Aidha mafunzo hayo yalifundishwa kwa vitendo na nadharia kwa lengo la kurekebisha kasoro zinazojitokeza wakati wa utoaji wa huduma na kuwanoa zaidi watalaamu hao waweze kuendana na wakati katika kutoa huduma bora za afya ya mama na mtoto.
Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Bw.Makwaia Makani alisema wahitimu watumie vizuri elimu na ujuzi walioupata ili kuendelea kutekeleza vyema lengo la milenia la kupunguza vifo vya kina mama na watoto.
Kwa Mjibu wa Gazeti la Habari Leo, Ijumaa tarehe 23, Septemba, Rais Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo mbili kutokana na mchango wake mkubwa katika afya mama na mtoto. Tuzo ya kwanza imetolewa na Taasisi ya Kijamii ya Umoja wa Mataifa (UN Foundation) na tuzo ya pili ilitolewa katika makao makuu ya Soko la Hisa la marekani (NACAQ) ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani baada ya lile la New York.
Wahitimu wa mafunzo hayo ni wauguzi na madaktari wanaofanya kazi katika kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto cha Idara ya Magonjwa ya Akina Mama, Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mafunzo haya yalidhaminiwa na Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...