Na Abdulaziz Video.

KUTOWAJIBIKA ipasavyo kwa Taasisi zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi nchini ni miongoni mwa sababu zinazochangia kushamiri kwa unyanyapaa miongoni mwa jamii.

Changoamoto hiyo imetolewa jana na Afisa Habari wa shirika lisilo la kiserikali la PACT Tanzania katika mafunzo ya unyanyapaa dhidi ya watoto na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, wakati akitoa mada kwenye mafunzo hayo yaliyojumuisha waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Mafunzo hayo yanaratibiwa shirika lisilo la kiserikali la Pact Tanzania kwa ufadhili wa mfuko wa Rais wa Marekani ambapo yanafanyika kwa siku tano kwenye ukumbi wa Morogoro Hoteli mjini hapa.

Alisema kuwa pamoja na wahisani kutoa fedha nyingi kwa asasi hizo ili ziweze kutoa elimu kwa jamii dhidi ya mapambano dhidi ya ukimwi na unyanyapaa nchini, zimekuwa zikishindwa kufanya hivyo hali ambayo imechangia kushamiri kwa unyanyapaa hasa dhidi ya watoto na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.

“Ukweli ni kwamba hizi asasi zinazopambana na ukimwi hazitekelezi wajibu wake ipasavyo ndio maana tatizo la unyanyapaa linazidi kushamiri kila kukicha,sasa hii ni changamoto kwao na sisi wadau wa vita dhidi ya ukimwi na unyanyapaa kwamba tubadilike na kuwajibika kwa kutoa elimu ya athari zake hali ambayo inaweza kusaidia kupunguza na kumaliza unyanyapaa hasa kwa watoto na wagonjwa wa ukimwi” alisema Manyama.

Aliongeza kuwa matokeo ya utafiti uliofanyika tangu mwaka 2001 hadi 2003 yanaonyesha kuwa unyanyapaa upo kwa kiwango kikubwa kwenye jamii hususani kwa katika makundi na maisha ya kawaida ya watu ambapo unazorotesha jitihada za kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini.

Akichangia katika mafunzo hayo, Mwandishi wa habari Mwandamizi, Felix Mwakyembe, alitilia shaka takwimu zinazotolewa na Serikali juu ya maambukizi ya ukimwi kutokana na hali halisi yanayokutana nayo kwenye maeneo yanayoelezwa kuwa maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi.

“ukienda maeneo kama vile Makete hali halisi sio kama takwimu zinavyoeleza,sasa ipo haja takwimu hizi nazo ziangaliwe upya kwani tofauti na hivyo inawezekana watu wanazitumia kama miradi ya kutekeleza malengo yao” alisema Mwakyembe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...