Mbunge wa viti maalumu CCM mkoani Lindi, Bi Zainab Kawawa akikabidhi hundi kwa Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi KAWAWA iliyotolewa na Mfuko wa Penseni kwa watumishi wa Umma(PSPF)kwa ajili ya ukarabati wa madarasa matano likiwemo alilosoma Marehemu Mzee Rashid Kawawa
Mbunge wa viti maalum akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule hiyo.
Darasa ambalo Waziri mkuu wa kwanza Tanzania,Marehemu Rashid Kawawa alisoma wilayani Liwale,Mkoani Lindi.
Mlezi wa Shule ya msingi kawawa ambae pia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi,Bi Zainab Kawawa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Mfuko wa Penseni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Kwa kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanzania,Marehemu Rashid Mfaume Kawawa alioutoa wakati wa uhai wake,Leo Umekabidhi jumla ya shilingi Mil 12 kwa ajili ya kukarabati vyumba vitano vya madarasa likiwemo darasa alilosoma Mzee Kawawa katika shule ya msingi Kawawa iliyopo wilayani Liwale Mkoani Lindi.
Kutolewa kwa mchango huo kutawezesha kupunguza kwa msongamano wa wanafunzi wa shule hiyo ambapo kwa sasa darasa moja huwa na watoto wasiopungua 60.
Akikabidhi hundi hiyo kwa Mwenyekiti wa shule hiyo kwa niaba ya shirika hilo,Mbunge wa Viti maalum,Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Kawawa alishukuru kwa mchango huo na kuitaka kamati ya shule hiyo kukamilisha kwa haraka ukarabati huo ili kupunguza msongamano katika vyumba vya madarasa yaliyopo.
Naye Mkuu wa shule hiyo,Bw Hashimu Libena licha ya kushukuru kwa msaada alieleza jinsi msaada huo utakavyosaidia shule hiyo yenye historia Nchini Ikiwa pamoja na kuinua kiwango cha taaluma ambapo piaalibainisha kuwa shule hiyo kwa mwaka 2010 wanafunzi waliofanya mitihani ya darasa la saba walikuwa 164 na waliofaulu ni 159.
Kufuatia tukio hilo la kukabidhi hundi hiyo,Mwenyekiti wa kijiji cha Mpirani,Bw Mohamed Ally akifunga hafla hiyo, aliiasa kamati ya shule kuzitumia pesa hizo kama zilivyopangwa nae kuhaidi ufuatiliaji wa pesa hizo.
Shule hiyo ya msingi Kawawa yenye wanafunzi 1475 alianza miaka 70 iliyopita kwa muundo wa darasa la kwanza hadi la nne ambapo Mbunge wa Kwamza wa jimbo la Liwale na Waziri mkuu wa Kwanza wa Tanzania alipataelimu yake ya awali katika shule hiyo iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Liwale Uper School.
Ndugu Rashid Mfaume Kawawa hakuwa Waziri Mkuu wa kwanza bali wa pili baada ya Waziri Mkuu wa kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kujiuzulu wadhifa huo tarehe 22/1/1962 ili kwenda kukiimarisha chama cha TANU.
ReplyDelete