Jumuiya ya Watanzania United Arab Emirates (TAE) kwa masikitiko na huzuni kubwa inatoa SALAM ZA RAMBIRAMBI kwa wafiwa wote ambao wamepoteza NDUGU, WAZAZI, WATOTO, WENZA WA MAISHA, JAMAA NA MARAFIKI kwa msiba mkubwa uliowafika. Rambirambi hizi ziwafikie Viongozi wote na Wananchi wote wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jumuiya inatoa pole kwa majeruhi na walionusurika kwenye ajali hii.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu awajaalie ahueni ya haraka majeruhi wote.

Tunaungana na Watanzania wenzetu katika maombolezo huzuni na kuwatakia rehema na amani ya Mwenyezi Mungu wale wote waliofariki.


Issa Majid Maggidi

Naibu KatibuJumuiya ya Watanzania UAE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...