Assalam aleykum kaka michuzi.

Kwanza nakupongeza kwa kutu pasha habari sie tulio nje ya tanzania haswa ktk msiba mzito wa ajali ya boti

Napenda kutoa pole kwa wote waliopotezewa na wapendwa wao ktk ajali hio na pia nawaombea kwa Mungu awape nafuu wale walionusurika. 

pia nampongeza mheshimiwa Rais kwa kuharisha safari yake ya nje ya nchi na kujumuika ktk msimba mzito ulioikumba Taifa bila kuwasahau Dr shein na watu wa visiwani kwa kua pamoja pia Mh zito kabwe kwa kusema ukweli kuhusu vituo vya tv kutoonyesha habari za ajali badala yake wanapiga muziki afadhali hata wangepiga nyimbo za dance ambazo zina maudhuhi ya kuwapa pole wafiwa nawapongeza clouds kwa siku ya leo tar 11 sep wanajitahidi kupiga nyimbo za huzuni muda si mrefu nilisikiliza nyimbo ya kifo iliopigwa na matimila. 

Hajabu nyingine hawa wezetu wa miss tanzania na wadhamidi wao hivi wameshindwa kabisa kuhairisha mashindano yao mpaka baadae?badala yake wameendelea na mashindano km kawaida hivi kweli miss wetu ataweza kubaikiwa kuchukua taji la dunia kwa hali hii? 

km ktk ajali ya juzi wangekuamo ma miss wawili tu sidhani kama yangenyika mashindano kwa jana almuhimu hakuna binadamu alie kamili na mtu/watu hujifunza kutokana na makosa inachotakiwa wajipange na wawaombe radhi wananchi kwa yote yaliotokea.

Nawatakia marehemu wote mapunziko mema,majeruhi wapate ahueni na wafiwa wawe na subra ktk kipindiki hiki kigumu cha msiba Inshallah wote tunapita njia hiohio ya kifo tutatofautiana masaa,siku na sababu

Ahsante

A.Mdidi

South east,London

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...