1.   Jumuiya ya watanzania ugiriki inachukua nafasi hii kutoa pole na kuelezea masikitiko na huzuni za watanzania wote wa hapa  kwa ndugu na jamaa wa marehemu.Mwenyezi Mungu aziweke roho zao peponi.
2.   Kwa wale waliookoka,tunamuomba Mola awakutanishe na familia zao wakiwa katika hali ya afya,utulivu na usalama.
3.   Katika mkutano wa wanajumuiya (tuliokuwa tumeshaupanga kufanyika leo 10/09/2011) tutawakumbuka kwa dua wale wote waliofariki na wale wote waliookoka katika ajali hii.
4.   Tunaamini viongozi wetu wana uwezo mkubwa na wa hali ya juu wa kufuatilia na kujua sababu halisi za ajali na kuhakikisha ajali kama hii haitokei kirahisi katika siku za usoni.

 Kayu Ligopora
Katibu wa jumuiya 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bab kubwa Katibu unatuwakilisha vizuri sana watu wa umangani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...