Ndugu zetu poleni sana,
Rajabuhmblog(Fuel of the Future-FOF) tukiwa ni watanzania kama watanzania wengine popote pale duniani tumeguswa na tunaomshituko mkubwa kufuatia kupotelewa na jamaaa,ndugu na marafiki wapatao zaidi ya 192  waliokufa maji baada ya kuzama kwa MV. Spice Islander usiku wa kuamkia jana (10-09-2011) katika pwani ya Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja.
Rambirambi zetu tunazipeleka mojakwa moja kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, Dr.Mohamed Shein pamoja na wafiwa wote waliopotelewa ndugu na jamaa. Tunaungana na watanzania wenzetu katika siku hizi tatu za maombolezo ambazo zimetangazwa na Marais wetu ambapo blogu hii pendwa ya "FUEL OF THE FUTURE-FOF" ipo pamoja kuwafariji wafiwa kwa njia yoyote ile ambayo itakayowapa nguvu na subira wafiwa wote na si vinginevyo. Hili ni janga kubwa sana kwa taifa letu hasa ukilinganisha uwezo wetu wa kukabiliana na majanga makubwa kama haya bado ni mdogo sana.Mungu aziweke mahali pema roho za marehemu wote waliofariki kufuatia janga hili kubwa,Ameen
Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania.
Stockholm
Sweden

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...