Uongozi na wanachama wa Jumuiya ya waTanzania nchini Uholanzi (TANE), umepokea habari za kuzama kwa Meli ya MV Spice Islander kwa masikiko na majonzi  makubwa. Tumeuzunishwa mno kwa  idadi ya vifo na majerui waliotokana na ajali hiyo.

Jumuiya, inaungana na waTanzania  kwa kutoa salamu za pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar, ndugu wafiwa,  pamoja na majerui wa ajali.

Pia, Jumuiya inaungana katika maombolezo ya siku tatu kama ilivyotangazwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa.


Bulemo Francis Kweba
Mwenyekiti,
Tanzania Association in the Netherlands. (TANE)

11 September 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...