UmojaPhone.com na uongozi wake tunapenda kutoa salam za rambirambi kwa ndugu na jamaa wote ambao kwa namna moja au nyingine watakuwa wameathirika na janga la hivi karibuni la ajali ya meli ya MV Spice Islander. Tunawashukuru watanzania wote kwa kuwa watulivu na kuimarisha amani nchini kwetu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
UmojaPhone.com iko tayari kusaidia gharama za mawasiliano ya simu kwa mtanzania yoyote aishie nje ya Tanzania na ambaye anashida ya kupata mawasilliano na ndugu kule nyumbani kwa kipindi hiki. Kwa taarifa za kina wasiliana nasi kwa kutuma barua pepe kwenda
Mbona Tanzania kupiga simu ni ghali kuliko Kenya au Uganda?
ReplyDeleteJibu kwa nini kupiga simu Tanzania inakuwa gharama kuliko majirani zetu Kenya na Uganda ni kuwa makampuni yetu ya simu TZ yanatoza viwango vya juu kwa simu zinazoingia kutoka nje tofauti na viwango vinavyotozwa na majirani zetu.
ReplyDeletePengine ni wakati sasa TCRA ikaliangalia hili.