Kwa niaba ya Jumuiya ya Wanafunzi Wanaosoma Shahada Ya Kwanza Ya Sosholojia (Bachelor Of Arts in Sociology) ya Chuo Kikuu Cha Dodoma inapenda kuwapa pole watanzania wenzetu wa Tanzania Bara Na Visiwani Zanzibar kwa msiba mkubwa uliolikumba taifa

Wanafunzi tunaosoma Shahada ya Kwanza Chuo Kikuu Cha Dodoma Tunapenda Kutoa Salamu Zetu Za Rambi Rambi Kwa Raisi Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete na Raisi Wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein Kufuatia Msiba Mkubwa uliolikumba Taifa Baada Ya Kuzama Kwa Meli Ya Spice Islanders Usiku Wa Kuamkia Jumapili ambapo Mamia ya Watu waliweza Kupoteza maisha na Wengine Kujeruhiwa Na 
Wengiwe wakiwa hawajurikani wapi walipo mpaka sasa.
Vilevile Tunapenda Kutoa Salamu Zetu Za Rambirambi Kwa Ndugu, Jamaa Na
Marafiki ambao wamepoteza Jamaa,Ndugu, Marafiki zao Katika Ajali hiyo
Kubwa iliyoikumba Taifa letu

Pia tunatoa Salamu zetu Za Rambi Rambi Kwa Mwanafunzi Mwenzetu LAHYA
Na Wengine Wote Walioguswa moja kwa moja Na Ajali Hii ya Meli
iliyopelekea Kupoteza maisha ya Watu wengi.

Wanafunzi Wote Tunaosoma Shahada ya Kwanza Ya Sociology na Shahada
Nyingine Za Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) tunaungana na Taifa kwa
pamoja katika wakati huu mgumu na pia tuko tayari kushirikiana kwa
hali na mali kuwafariji ndugu na jamaa kwenye msiba huu.

Mungu azilaze Roho Za Marehemu Mahala Pepa Peponi Amina na Mungu
Awabariki Na Kuwajaza Nguvu Ndugu, Jamaa na Marafiki Kwa Kuwapoteza
Wapendwa Wao

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

 Imetolewa Na

Josephat Lukaza

AFISA UHUSIANO

THE UNIVERSITY OF DODOMA SOCIOLOGY STUDENTS ORGANIZATION(UDOMSSO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. FRANK MAREALLESeptember 12, 2011

    hakika ni msiba mkubwa kwa taifa,ni muda wa kushikamana kwenyetatizo hili,kuwafariji na kuwapa pole wale wote walioguswa na janga hili.pole sana mwanafunzi mwenzihakika ni msiba mkubwa kwa taifa,ni muda wa kushikamana kwenyetatizo hili,kuwafariji na kuwapa pole wale wote walioguswa na janga hili.pole sana mwanafunzi mwenzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...