Na Salama Njani,  Habari-Maelezo Zanzibar

Timu ya Wanajeshi 22 ya Uokozi kutoka Afrika ya Kusini imewasili Zanzibar leo alfajiri, kwa ajili ya kuendelea kusaidia kazi ya uokozi katika ajali ya meli iliyotokea juzi Zanzibar

Timu hiyo ya waokozi  12  ni waokoaji, 4 ni Madaktari, na waliosalia ni wafanyakazi wa ndege hiyo ya Jeshi iliyowaleta timu hiyo,

 Kuja kwa timu hiyo ya jeshi kutoka Afrika ya Kusini kunatokana na ombi la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK Jakaya Kikwete ,kwa Serikali ya Nchi hiyo, kuja Tanzania kutoa msaada wa uokozi.

 Timu hiyo ya jeshi la Afrika ya Kusini imekuaja na vifaa vyake kamili vitakavyosaidia kazi hiyo ya uokozi .Mbali na kazi hiyo itatoa ripoti ya kuishauri Serikali katika utaratibu mzuri wa kukabiliana na maafa kama hayo.

Timu hiyo ya watu 12 ya uokozi kutoka Afrika ya Kusini itashirikiana na waokozi wa jeshi la wananchi wa Tanzania, KMKM,na wananchi katika kuendelea na kazi ya uokozi.

Wakati huo huo Makamo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, amepokea misaada mbali mbali kutoka kwa vyama vya siasa, taasisi za dini na Mashirika.

Chama cha Demokrasia Tanzania (CHADEMA) kimetoa shilingi millioni tano, zilizowasilishwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, Bank ya CRDB imetoa jumla ya shilingi milioni kumi,ambazo zimewasilishwa na mkurugenzi masoko wa Benki hiyo Tully Esther Mwambapa

Wengine waliotoa msaada ni pamoja na umoja wa vijana wa CCM Zanzibar umetoa jumla ya shlingi laki sita, kanisa la Anglikan Zanzibar wametoa shilingi laki tano na Jumuiya ya umoja wa Kiislamu Zanzibar ( UKWE) wametoa jumla ya shilingi laki tano.

Wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo wamepewa mapumziko maalum kwa ajili ya kushiriki katika Dua ya pamoja katika kuwaombea waliofariki ajali ya meli ya Spice Islanders hapo juzi, dua amabayo itasomwa katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar jioni hii.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
12/09/2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...