Asalaam aleykum
Inna Lillahi wa Inna Illahi Rajuun
Kwa manoujua vizuri mji wa London, Barking ni kitongoji ndani ya jiji la London ambako nathubutu kusema tumepoteza ndugu zetu wengi zaidi kwenye Janga hili kutokana na ukweli wa wakaazi wengi wa Unguja, Pemba na Pwani kuwa ni makaazi yao. Na zaidi hapa kwenye Magorofa yetu ya Gascoigne (Michenzani) ambako kuna vilio familia zaidi ya 14.
Tunapenda kuungana na wenzetu nyumbani kwenye msiba huuu na kumwomba Allah awaepushe na adhabu za kaburi na moto waliotangulia mbele ya haki kwani twafaham kuwa sote tuko njiani.InshaAllah atupe wepesi katika kipindi hiki chenye mihani mkubwa na inshaAllah tutawaaribu watu wa AL NOOR Community Centre (jirani na market) lini tutafanya Khitma kuwaombea wenzetu waliotutangulia
wabillahi Taufiq
A. Mwinyimbegu (Katibu mwenezi)
(kwa niaba ya wa Wa Tanzania waishio Barking, Thamesview & Dagenham


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...