Jumuiya ya wanafunzi wa chuo tajwa hapo juu wamepokea kwa masikito na majonzi makubwa ajali ya Meli ya Mv Spice Islander iliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 10/09/2011 na kusababisha majeruhi na vifo vya watanzania wenzetu.
Wanajumuiya wote pamoja na wanafunzi wenzetu kutoka nchini Kenya tunaungana kwa pamoja kutoa salaam zetu za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao wamepoteza wapendwa wao. Salaam za pole ziwafikie pia viongozi wetu wa Kitaifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Dkt. Ali Mohamed Shein na watanzania wote.
Ni kipindi kigumu kwa wafiwa na taifa kwa ujumla. Jumuiya inachukua fursa hii kuomba Mungu awape nguvu katika kipindi hiki cha majonzi.
Jumuiya pamoja na marafiki zetu hapa chuoni tunawaombea majeruhi wapone haraka na kurejea kwenye shughuli za ujenzi wa taifa letu. Pia tunawaombea marehemu wote wapokelewe mahali pema peponi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Amina.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Emmanuel J. Bwasiri
Katibu wa Jumuiya (Wits).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...