Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji na kuwapongeza wananchi wa kijiji cha Nungwi kufuatia juhudi zao za kujitolea kuwaokoa watu waliopata ajali katika meli ya MV.Spice Islanders iliyotokea juzi usiku.Meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kwenda Pemba amapo watu zaidi ya 200 wanahofiwa kufa maji.Abiria 602 wameokolewa wakiwa hai.
Balozi wa Marekani nchi Tanzania Alfonso Leinhardt akimfariji Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia ajali ya meli ya Spice Islanders iliyotokea huko Nungwi, Unguja juzi usiku ambapo watu zaidi 200 wamepoteza maisha na wengine 602 kuokolewa wakiwa hai (picha na Freddy Maro).


Nami najiunga na wenzangu kutoa rambirambi kwa wafiwa na kuwaombea waliofariki dunia katika ajali hiyo wapumzike kwa amani. Hata hivyo, naomba kuchukua fursa hii kuomba mamlaka husika zichukue hatua kali za kisheria kwa wamiliki/wasimamizi wa meli hiyo walioruhusu abiria wazidi na mizigo isheheni kupita kiasi. Nasema hivyo kwa kuwa wengi wetu tulio wa kanda ya ziwa bado tunakumbuka tamaa ya wamiliki/wasimamizi wa ferry iitwayo MV BUKOBA ilivyosababisha zaidi ya watu 700 kuzama Ziwa Victoria. Mugisha.
ReplyDelete