Nimeguswa sana na salaam zenye maoni za Mhe. Zitto kuhusu maafa yaliyotokea Zanzibar na mambo mengine yaliyoendelea ambayo yesingefaa kuendelea wakati huo. Labda ilikuwa ni ukosefu wa taarifa za uhakika.Huwezi kujua.
Lakini hapa Arusha, kwa wakati huo, sisi tulikuwa na ugeni mzito wa watu kama 120 wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na mawaziri wa Zanzibar wapatao kumi wakiongozwa na Spika wa Baraza Mhe. Amer Pandu Kificho. Walikuwa Arusha kama wageni wa Arusha Wazee Sports Club. Walifika Alhamisi na walitegewa kuondoka Jumatatu hii.
Siku ya pili, yaani Ijumaa, tuliwatembeza hapo kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Nelson Mandela Pan African Institute of Science and Technology, hapo Tengeru. Taasisi hii ni ya ngazi ya kimataifa ambayo itachukua wanafunzi na watafiti wa kuanzia degree ya Masters na Phd tu. Inaanza masomo mwaka huu.
Kwa kweli ni taasisi ambayo inaiingiza Tanzania katika ulimwengu wa technologia ya kisasa na utafiti wa kisayansi wa hali ya juu.
Baada ya hapo tuliwapeleka kampuni mpya ya Hughes Motors ambayo ianuza magari ya Ford na kuservice na kutengeneza magari mbalimbali. Hii kampuni ipo hapo Usa River na tulishangaa kuona magari mengi sana kutoka sehemu mbalimbali nchini na hasa Dar es Salaam yaki-servisiwa na kutengezwa hapo.
Jumamosi wageni walikuwa watembelee mbuga ya wanyama ya Tengeru na Jumapili ilikuwa tucheze michezo na klabu yetu ikiwemo mpira wa miguu hapo General Tyre, kabla hatujawaaga ili warejee Zanzibar jumatatu.
Lakini haikuwa hivyo kwani habari za msiba tulizipata asubuhi hiyo ya Jumamosi. Kazi ikawa kuhakikisha wajumbe wote na mawaziri wanasafirishwa kurudi Zanzibar kushiriki katika msiba huu mkubwa. Tunashukuru Mungu walifika wote salama.
Makampuni yaliyokuwa yemedhamini michezo hiyo ambayo ni TBL, Vodacom na Bonite Bottlers yaliridhia kusitishwa kwa shughuli zote.
Na sisi wanachama wa Arusha Wazee Sports Club, tunaungana na Watanzania wengine katika msiba huu, na tunatuma rambirambi zetu kwa wananchi wa Zanzibar na hasa kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi tukieleza mshituko na masikitiko yetu kwa msiba huu mkubwa.
Na leo hii tumewatuma wajumbe wetu wawili, Bwana Aatsa, kutoka Cameroon, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Klabu na Mama Stella,Mtanzania, Mjumbe, kuelekea Zanzibar kuwakilisha salaam zetu na kushiriki kikamilifu katika msiba huu.
Mungu aziweke pema Roho za wote waliopoteza maisha yao katika ajali hii.
Amen
Danford Mpumilwa
Mwenyekiti
Arusha Wazee Sports Club
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...