Kwa niaba ya wanafunzi wa Tanzania wanaosoma International Islamic University Malaysia, tunapenda kuungana na ndugu wa marehemu na wananchi wa Tanzania kwa ujumla ili kueleza majonzi na masikitiko yetu makubwa kutokana na vifo vilivyo sababishwa na ajali ya kuzama kwa MV Spice Islander katika eneo la Nungwi bahari ya Zanzibar usiku wa tarehe 10 September 2011.

Tunamuomba Allah (S.W) aliye mwingi wa rehema kwa viumbe vyake, azilaze roho za marehemu wote katika mahali pema pamoja na kuwaondolea adhabu za kaburi katka malazi yao na pia kuwaombea afya njema majeruhi wa ajali hiyo. Mwisho Allah (S. W) awape subira wale wote walioathirika na msiba huo, ÓMÔN.

Wanafunzi wa IIUM

Malaysia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...