Mshambuliaji wa timu ya Simba,Haruna Moshi 'Boban akiipangua ngome ya Azam FC kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara leo.Timu hizo zilitoka suruhu ya bila kufungana.
Mshambuliaji wa Simba, Patrick Mafisango (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Azam, Erasto Nyoni
Golikipa wa Azam FC akiokoa moja ya hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Simba uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka suruhu ya bila kufungana. Kushoto ni Mshambuliaji wa Simba, Garvas Kago.
Mashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao wakati wa mchezo wao dhidi ya Azam FC. Timu hizo hazikufungana.


Hawa TFF hawajui kama taifa lipo kwenye msiba? Hata hiyo ligi ya Uingereza husimamishwa ikitokea maafa nchini mwao itakuwa ligi koko ya bongo!!
ReplyDeletekaka michuzi.simba jana walikalia kuti kavu.ila naona picha harakati za simba za azam sizioni.
ReplyDeleteYALE YALE SASA HAWA TFF HAWAJUI KM KUNA JANGA LA TAIFA AMA?WAMEONA HASARA KUPROSPOND MECHI,HAYYA TUTAFIKA TU!!!!!!.
ReplyDeleteKatika matukio ya majanga ya kitaifa kama haya shughuli za kimichezo sio lazima zisimamishwe bali huwa kunakuwa na dakika kadhaa za maombi ambapo kila mtu hapo uwanjani hukaa kimya na kuwaombe dua wafu. Badala ya hapo mchezo unaendelea kama kawaida. Ikumbukwe mkusanyiko mkubwa kama huo huleta muungano wa kimaombi!!! Acheni kuropoka kama hamjui michezo!
ReplyDelete