![]() |
| Mh. Zitto Kabwe. |
Ndugu zangu wanawavuti salam kwenu, naomba mnifikishie ujumbe huu kwa watanzania. Shukrani zangu za dhati.
(Nimeandika makala haya nikiwa katika Benchi la Hospitali ya Mnazi Mmoja hapa Zanzibar. Mniwie radhi kama kuna spelling mistakes kwani nilitaka hisia zangu ziwe as raw as possible -Zitto Zitto and not Zitto a politician).
Jana asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu 2000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba.
Habari hazikuwa za uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa Televeshini ya Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii. Habari zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa habari nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili tuweze kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.
Habari zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki wa Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa Umma kuhusu msiba huu.
Watanzania waliokuwa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa na hasira sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya ajali hii. Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake wakikatika viuno na hata ngoma za asili. 'Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu inachoonyesha' yalikuwa ni maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu aliponipigia kuonyesha kusikitishwa kwake na kituo hiki.
Mpaka jioni tulikuwa tumepata taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa wamepoteza maisha. 570 hivi walikuwa wameokolewa. Binafsi nilipotembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti aliyeitwa Leyla, akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla alipona, aliokolewa. Nilimwambia leyla atapona na kurudi Shuleni.
Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa. Napenda kuwapongeza sana waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na vijiji jirani, wamiliki wa mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda kuokoa watu na wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi hii kubwa ya kuokoa.
Kwa kweli tumeokoa watu wengi kuliko ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi sana, ilitulia na kuonyesha uongozi dhabiti katika juhudi za uokoaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko Canada, ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini Rais aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi hiki. Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta. Akatangaza siku 3 za kuomboleza. Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona hasara kubwa kuahirisha shindano la Urembo usiku huo.
Wangepata hasara! Hata wafadhili wao Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom ambao miongoni mwa waliofariki wamo wateja wa vodacom, waliendelea na shindano hili. Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea marehemu wetu. Nimeamua kutotumia simu ya ngu ya Voda kwa siku nzima, sina njia ya kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao japo kwa siku moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa kutojali msiba huu kwa Taifa.
Misiba huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio kubwa kwa Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa limeshindwa jaribio hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi hiki. Nataraji wakubwa wa Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi watawajibika au kuwajibishwa!
Jumla ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya Abiria 800! Asubuhi ya jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo wa Boti la MV Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12.
Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria. Natumai mara baada ya kumaliza
maombolezo haya ya siku tatu Wakuu wa Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa.
Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu Hamad Masoud wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika wenyewe kwa kujiuzulu.
Kufukuzwa kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni somo kuwa hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama hii.
Mwenyezimungu atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa letu. Alaze roho za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu wa haraka majeruhi wetu.
Zitto Kabwe.



Katika viongozi wote.....Mh Ztto Kabwe naona kidogo ana utu....Zitto Kabwe for uraisi 2015.
ReplyDeleteWewe Mtu una akili na hisia za ajabu na inaonyesha wewe ni Kiongozi Imara tatizo uko chama ambacho sio!!Ninayathamini maoni yako na kuyakubali.Hiyo simu Ya VodaCom Igomee moja kwa moja.Hii kwa watu wengi imeonyesha kuna aina ya Ubaguzi.MV Bukoba ilipewa coverage kubwa mno mpaka visiwani iweje hili la Zanzibar?!
ReplyDeleteMkereketwa
Tandika Mabatini
Nashukuru sana Ndugu Zitto kwa tathimini yako ya haraka na yenye ukweli mwingi tu. Kwakweli sipo nchini ila nimejitahidi sana kufuatilia taarifa hizi mara tu nilipozipata mtandaoni toka asubuhi ya jana. Ukweli Vyombo vyetu vya habari sijui havina vifaa au hatuna watafiti wa kina katika matukio kama haya inasikitisha kuona kuwa TBC hawakuwza kuwa na coverage nzuri ya tukio hili lakusikitisha. Mbaya zaidi ni kuhusu Shindano la miss Tanzania. Kwakweli imeonyesha ni jinsi gani Vodacom kama mdhamini mkuu na wadhamini wengine kuendelea na shindano wakati huu wa msiba mkubwa wa watanzania wenzetu. Ninaamini kabisa katika Meli hiyo kama ulivyotanguli kusema kuna wateja wengi tu wanaotumia mtandao huo katika hao watu 500 tu wanachangia pesa nyingi sana kuliko hata shindano lenyewe. Mimi pamoja na watanzania wenzangu tulioko seoul tunasikitika na kutoa salam zetu za pole kwa taifa, jamii na familia za watanzania wenzetu waliopata ajali na kupoteza maisha yao. Mungu awape nguvu ndugu na jamaa wote na azilaze peponi roho za marehemu. Amina
ReplyDeletemwaky
mara nyingi nimekua sikubaliani na mh.zitto hasa katika miaka ya hivi karibuni lakini kwa hili zitto amejipambanua kuwa miongoni mwa wanasiasa shupavu wasioogopa kusema ukweli hata kama ukweli huo utawaudhi baadhi ya watu tunaowaheshimu wakiwamo wafadhili ama wadhamini wetu,hongera bwana zuberi kabwe zitto,naungana nawewe kuwalilia ndugu zetu,machozi yamegubika kope za macho yangu...simanzi moyoni,mbele yao nyuma yetu wote walioangamia katika ajali hiyo mbaya,najua mengi yatasemwa sana lakini mwisho wa siku kazi ya mungu haina makosa
ReplyDeleteMhe. Zitto, tafadhali acha kujipendekeza na kujitafutia umaarufu. Uozo wa Tanzania umejaa kila sehemu, hata huko Bungeni mliko.
ReplyDeleteukweli ni kwamba wamechemsha naungana mh Zito kwa hili wawajibishwe
ReplyDeleteBIG UP MHESHIMIWA ZITTO KABWE(na CHADEMA KWA UJUMLA),KWA KUUJALI UTU ZAIDI KWA KUVUNJA SHUGHULI ZAKO NA KUFIKIA ENEO LA AJALI.UKILINGALISHA NA WALE KINA MKAPA KULE IGUNGA.KIULINGANO TU INAONEKANA KABISA KM CHAMA TAWALA HAKINA UTU WALA HAKIMJALI MPIGA KURA ILA KULA YAKE TU NA KISHA KUMBEZA tupeni kura zenu then mtabaki sana gizani kwanza mmesha zowea kiza na hata mkifa putelea mbali.
ReplyDeleteZitto you are my role model kwakweli katika viongozi wa taifa hili kaka wewe mimi nakukubali saana na kazi zako zote nje na ndani ya Bunge nazikubali saana ningekuwa ninauwezo basi kaka siku moja hata kukupa
ReplyDeletenchii hii uiongoze wala nisingekuwa na hiyana hongera saana kaka Mungu akujalie siku moja uje uongoze taifa letu
Wewe unaongea nini, tokeni bungeni muone wananchi wanavyosafiri kama magunia ya dagaa nyie mpo kwenye mashangingi na mindege ya bei mbaya. Mmeanza kublame kwa watu wasiohusika. Instead of saying anything about waziri wa uchukuzi wewe unaongelea TBC, UNAKAMATA DAGAA WAKATI KUNA PAPA. Ama kweli watanzania tumelala.
ReplyDeleteNakubaliana 100% na mheshimiwa zitto.
ReplyDeleteKuna watu ambao wameajiriwa na wanalipwa mishahara ya bure kwa kodi zetu watanzania. Nawazungumzia hao SUMATRA wa Zanzibar. Watanzania wenzetu wamepoteza ndugu jamaa na marafiki na pengine watu waliokuwa wanategemewa sana katika familia zao. Watoto wengine watabaki mayatima kwa sababu ya watu kutokuwajibika na kutimiza majukumu yao. Tabia hii sasa imeanza kuota mizizi hata katika sekta nyingine za umma na ni hatari sana hata kwa mustakabali wa taifa letu. Mimi nashauri waziri anaeshughulikia masuala ya usafiri wa zanzibar aanze kuchukua kuonesha collective responsibility. Lakini zaidi hao watendaji wakuu wa SUMATRA ya Zanzibar sio tu wafukuzwe kazi mara moja bali wafikishwe mahakamani kwa kutokuwajibika
Tujifunze kuwajibisha kwa uzembe wa watu tunaowapa kazi ya kusimamia sekta za umma ambao wanakula mishahara ya bure matokeo yake ndio kama haya.
Nawasilisha
Ndugu Mheshimiwa asante sana kwa hisia zako lakini inavyoelekea katika habari yote ni unajifagilia kisiasa na kutaka kutoa lawama kwenye vyombo vya habari! Nafikiri sasa hivi sio wakati wa kuonyesheana vidole kinachotakiwa ni kuokoa waliozama, na kuwahudumia waliojeruhiwa. Ni kipindi kigumu sana kwa taifa kwani familia nyingi zimepoteza wapendwa wao. Ni wakati tunaotakiwa kuwaombea wote walioathirika na janga hili ili Mungu awatie nguvu na ujasiri katika kukabiliana na wakati huu mgumu. Ninaona tusitumie vyombo hivi kwa faida za kisiasa na kutaka kujionyesha kana kwamba kuna watu baadhi wanaijali nchi hii na wengine hawaijali. Haya matatizo ya usafiri yapo kwa miaka mingi na hakuna aliyejigusa mpaka pale tatizo limetokea ndo watu wanakurupuka na kutaka watu wengine wawajibishwe. Tusitoe hukumu mapema acheni uchunguzi ufanyike kwanza na hii itafungua milango mingine na kuiwezesha serikali tawala na viongozi wake wote wa upinzani na sio wa upinzani kufuatilia vyombo vyote vya usafiri na kuhakikisha kwamba vinaendeshwa katika mazingira ya kulinda usalama wa raia.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu awapumzishe katika raha ya milele wale wote waliotangulia mbele za haki. Awaponye kwa haraka wale wote waliomia na awatie nguvu wale wote waliowapoteza wapendwa wao.
AMEN MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
Mdau USA
Ajali ni Ajali tu, Biashara yenyewe wawekezaji ni Wanasiasa! Meli hii imekuwa ikila mzigo mzito ziku zote> Lakini waswahili wanasema siku za mwizi ni arobaini na hii ndio siku yenyewe.
ReplyDeleteMv Kigamboni inakula mzigo kila siku na arobaini yake inakaribia
Mabasi mengi yanasafiri mzigo mzito kuliko ipasavyo na wamiliki ni baadhi ya wanasiasi!
Tanganyika and Zanzibar tunarudi nyuma sasa.
We need Nyerere Family to take over this country ! Where are you Madaraka??????
Nadhani Mheshimiwa zitto umeongea kila kitu kwa uwazi hasa ulipoachana na siasa na kuongea kama wewe. Nilitazamia watanzania wangesoma message inside your message wangejua kwa kiasi gani umekuwa open na umeguswa na msiba huu. Kifupi mimi si mshabiki wako ingawa mara kadhaa ukipatia nakupa big up.
ReplyDeleteTuwaombee maghfira wenzetu na pia subira kwa wahanga na wanafamilia. Lazima tutumie wasaa huu kujipanga vizuri zaidi. Nakumbuka miezi mitatu iliyopita meli moja kubwa ilizama nchini urusi na watu wengi walifariki na moja ya tatizo ni upakiaji wa kupita kiasi.
kwanini? lakini kwanini nasisi abiria hatusemi? Najua lawama za pamoja zinawakuta wakuu wenye mamlaka, lakini pia nasi huwa tunasumbua mamlaka. Mfano nimeshuhudia mara kadhaa trafic akizuia gari njiani or kituoni kwa mapungufu kadhaa, huwa sisi ni wakwanza kumuona mnoko na mwenye njaa. Nakumbuka wakati mtwara zinaenda mv mapinduzi na mv maendelea, tulikuwa tunalaumu sana tukiambia ticket zimeisha na wengine walikuwa wanaforce mpaka wasafiri.
Collectively tuna nafasi ya kujikosoa katika haya majanga.
regards,
G7
Bongo
kaka Zitto!alwayz I like u r analyisis kuanzia bungeni mpaka mtaani,makala yako ni Zitto Zitto kweli na imenisononesha sana na kujisikia vibaya especially jana nilipokuwa napita mitaa ya bar nyingi hapa Dar na kuona wananchi waki enjoy ukatikaji ya mauno ya warembo ambao waliokufa ni jamaa zao, na mchana huu nimetoka kuangalia matangazo ya TBC2 yenye bongo fleva motomoto na sio nyimbo za kuomboleza.swali ni hili ni kitu gani kitakachomwoyesha mtu kwamba taifa lipo kwenye maoombolezo kama pale anapofungua Tv na kukuta miziki ya ajabu au maungo ya dada zetu wa kike wakikatiza.RIP all who have dead.
ReplyDeletekabwe, sina uhakika kweli kama huna malengo ya kisiasa hapa, lakini kama ulivyosema hilo halipo umesema kama zitto.mimi nakukubali kupita maelezo kaka yangu, vibaya mno.una muono wa mbali halafu unajua kupanga cha kusema, kiufupi unaweza.nakushauri usiwe na papara za kuharakia ukubwa, cha kuomba hapa ni umri mrefu tu ili siku moja uwe rais wa nchi hii pengine kwa neema za mungu kupitia kwako angalau watanzania nao wakapata ahueni ya maisha hasa hasa wananchi wa hali ya chini. ushauri wangu kwako pia ni kutowajali miongoni mwa mafisadi ambao wanaponda kuhusu ukweli mtupu uliouandika maana hao ndio walewale kaka, wewe ni msomi, haina haja ya kuumiza kichwa kwa watu wachache.we angalia kati ya watu waliotoa maoni yao kuhusu makala yako aslimia 80 wamekubaliana na wewe na asilimia 20 ndio wanakupinga ambacho ni kitu kidogo mno..lakini pia nakushauri usiliache hili kama ninavyokufahamu, endelea kulichokonoa hadi hao uliowataja na wengine ambao hukuwataja wawajibike au la wawajibishwe....hongeza sana, unaweza!
ReplyDeleteMwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amina. Na wote mliofiwa (hasa ndugu na jamaa wa karibu) poleni sana, mwenyezi Mungu awajalie uvumilivu hasa katika kipindi hiki kigumu sana. Watanzania wote tuungane katika msiba huu, ni wetu sote.
ReplyDeleteMh Zitto angekuwa muwazi zaidi. Yeye ni mwanasiasa; kudai ametoa mchango aliotoa kama Ztto na sio mwanasiasa ni kutufunga kamba!
ReplyDeletenatuma hii msg kutoka nchini canada ukisoma gazeti la the sun na gazeti la toronto star ukisikiliza national news za hapa canada huna hamu ni jinsi gani wanavoona viongozi wetu wa nyasifa mbalimbali wasivyokuwa na uchungu wa wananchi kwani meli si ya abiria wakapakia abiria,hata hivyo wakazidisha,hilo swala litamaliza watu wasiokuwa na hatia ,umasikini wetu unatutosha watu wanakufa kwa njaa inafahamika ,lakini hili la uzembe kabisa kweli.sheria ifuate mkondo wake.nampongeza rais kuahirisha safari hata sisi wenyeji wake tulikuwa tukijiuliza kama kweli atakuja na hali ya nyumbani ni tete poleni sana yaani hapa nilipo nalia tu baada yakusikia taarifa hizi na ukizingatia ni za kizembe mno
ReplyDeleteNini Zitto usijifanye kama Gadafi,eti wawajibishwe wewe utakua tayar,ikitokea ajar kama hiyo katiko jimbo lako,mbona watu wanajazwa katika mitumbwi,boti kupita kias tena katk jimbo lako,umekauka kau,unawasema wenzako ili uonekane mwema kwa watu wa nje ya jimbo lako,kama Gadafi misaada mingi nje,ndan ovyo,na hata mabasi madogo yanayotoka manyovu_kigoma(noha)yanajaza kupita kiasi cjackia ukitetea,nauli kubwa kuliko bei za sumatra,nauli buku5 kilometa40,nyalubanda kigoma buku4 umekauka kau,wewe unataka hoja za nchi nzima ili uonekane(kwa malengo binafsi)swala la tbc+vodacom naunga mkono,mdau kutoka kalinzi_kigoma kaskazini
ReplyDeletevadacom hawana jabaya hata kidogo bali wewe zitto unachochea maovu ndani ya nchi inayoendeshwa kimazabe, vodacom wala haimo kabisaa. sijakusikia ukicoment kuhusu misaada ya vodacom inayotolewa kila siku kujenga mashule, kununua madawati na kudhamini michezo, leo umeona ni vyema kwako kutumia msiba huu kuwapaka matope watu wasio kuwa na hatia. uraisi hautafutwi hivyo, ajari imetokea ,cha msingi ni kutafuta kosa la ajali liko wapi basi,siyo kuleta siasa nyingi zisizokuwa na kichwa wala miguu. be carefuly man- huu muda wa leo ni wa majonzi na wala siyo muda wa kujitafutia umaarufu.
ReplyDeleteMaangalizo yako bwana mkubwa yanakubalika...ki msingi kama kweli TBC1 haikuwa ikionesha taarifa husika, basi kweli hawafai, na kulingana na mapendekezo yako kuhusu viongozi Zanzibar husika, nao wafukuzwe tu...bwana mkubwa rais afanye kusafisha pale. Nifanye kuwakumbusha tu swala la Gongo la Mboto...yalikuwa hayo hayo pia.
ReplyDeleteLakini kwa ujumla wake, maangalizo haya hayakuhitajika toka kwa kiongozi kama wewe kwa sasa bwana Zitto. Badala yake, ungezitumia aya zooote ulizoandika walau kutathmini na kuchakachua swala zima la usafirishaji na uchukuzi na kutoa mapendekezo yako baada.
Pamoja na uchafu wa viongozi walio wengi, kutoa maoni yao ni haki yao na ni wajibu wao hasa katika nyakati hizi...hivyo pamoja na nyakati kuhitaji tafakari tofauti toka kwako Zitto, hata kama ulikuwa unazungumza kama wewe, watoa maoni (hata kama ni haki hako kusema) haupaswi kumshurutisha huyu jamaa nae kwa kusema.
alioongea Zitto ni kweli ila sio kulalamikia TBC hawakusababusha ajali na maybe hawakua na mwakilishi eneo la tukio sio kosa lao pili kuzima voda yako haipunguzii voda chochote ni kweli kiubinadam imetoa na kuna mambo mengine hayazuiliki kuahirisha miss sio reason enough kuwa wamejali hata baada ya umiss naamini voda lazima watatoa rambirambi zao, wasingeweza kurisk jambo ambalo hawakupanga litokee na vilevile wanauwezo wa kusaidia jamii wanavyotaka tatu huwezi compare raisi na voda au tbc kwenye hili swala kuna wengine wanaweza kumudu na wengine hawzwezi
ReplyDeleteni ushauri tuu sina pingamizi na yeyote hapa,
asanteni
Naunga mkono kila ulilosema kaka Zitto.Maisha usipomthamini binadamu mwenzio,basi nawe hustahili kuthaminiwa.hAYO YA TBC1,VODACOM nimeyashuhudia kwa macho yangu.Nimeshinda nyumbani kwa sababu ninaumwa,nilishangaa sana kuona televisheni ya taifa ikiendelea na programs nyingine badala ya kuipa kipaumbele hii dharula tuliyoipata.
ReplyDeleteMAONI YANGU:TUSUSIE KUTUMIA HUDUMA ZA VODACOM,NA KWA WAE WANAOTANGAZA BIASHARA ZAO NA TBC1 WASITISHE NA WATAFUTE KITUO KILICHOONYESHA UBINADAMU LI IWE FUNDISHO KWAO
Michuzi,
ReplyDeleteKWANZA KABISA NAMPONGEZA MHESHIMIWA ZITTO KUSEMA UKWELI KUHUSU VODACOM, TBC KWA KUONYESHA JEURI NA KUTOJALI WATEJA WAKE NA TBC KUTUMIA VIBAYA FEDHA ZA WALIPA KODI. SASA WHAT'S NEXT??????
1. MICHUZI NAKUOMBA SANA KWA HESHIMA ZOTE WATAFUTE HAWA WAKUBWA WA VODACOM NA TBC1 ANGALAU UFANYE NAO INTERVIEW WARESPOND KWANINI WALIFANYA KILE WALICHOFANYA???? MAY BE WALIKUWA NA SABABU YAMSINGI KUENDELEA NAPROGRAM ZAO BILA KUJALI WATANZANIA NA WATEJA WAO.
2.I BET MICHUZI WAKIKUONA WATAKUKIMBIA MAANA RESULTS YA RESPONSE YAO ITAKIMBIZA WATEJA WOTE VODACOM NA KWENDA COMPAY ZA SIMU ZINGINE ZENYE KUJALI TZ CITIZEN. KUHUSU TBC1 KWA UPANDE WAO KUANZIA SUPERVISOR WA SIKU YENYEWE NA WOTE WALIOKUWA WAKIFANYA KAZI SIKU HIYO WAWAJIBISHWE AS WE SPEAK. HII UTUMIAJI MBAYA WA WALIPA KODI PERIOD!!!
Na mwisho Michuzi kama niliposema hapo juu PLEASE onesha how rue journalist how supposed to be to get those interview so that we can put this BOSSE's in RECORDS
GOD bless Tanzania!!
Amen
Nakupa tano mheshimiwa Zitto kwa maoni yako haya ya kibusara na kuheshimu ile mbaya big up mazee
ReplyDeletekuwajibika na kuwajibishwa ni sawa ingawa utamaduni huo iliishia na mzee rukhsa enzi hizo za utawala wa mwalimu. hapa katikati ni ujeuri tu wa walioboronga. labda tujifunze tena. inawezekana Zitto kauli hii ni yako kama Zitto na sina shaka imeipa uzito nafasi yako ya Zitto kama Politician. Je waliondelea na ulimbwende na kukata viuno na mipasho ni TBC1 peke yao? Kama wapo na wengine, kuna uzito kuwaunganisha katika lawama hii? Au labda kujumuisha wasiojali misba kama huu wakati mwengien ni jambo zito.
ReplyDeleteNdugu zanguni,
ReplyDeleteHivi hatupendi kusikia ukweli? Hata kama humpendi Kabwe alichosema ni cha msingi......Je tulitaka akisema nani? Kwa mantiki hii hata Akisema Rais Kikwete au akichukulia HATUA waliozembea tutasema anajipendekeza! Ukweli ni ukweli ukisemwa na CCM utabakia Ukweli.....ukisemwa na CUF utabakia UKWELI......Ukisemwa na CCM utabakia ukweli.....!Wazanzibari wakilalamika na kusema TBC haikulipa tukio hilo covarage inayostahili hatutasema Wazanzibari Jamani.......! Maana huo ndio ukweli.....! Watu wakilalama kuwa VODA haikuonyesha kukomaa kiutendaji huo utabakia Ukweli......! Hebu tusikipake na kukiangalia kila kitu katika macho ya siasa......! Hatutafika safari yetu ya kufumbua matatizo yanayotukabili
Hi Zitto, nakumbuka nilipoanza form one shule nani hii miaka ile niliona jina lako limeandikwa sehemu nyingi kama kumbu kumbu.Hata kwenye kuta, madawati,vyooni uliandikwa ushujaa wako wa kijinga na wa maana. Na rafiki yangu aliniambia kwamba huyu mwenye jina hili atakuja kuwa mtu msaada kwa taifa na jamii yake kwa ujumla. Leo nimesadiki kweli kweli umahiri wako
ReplyDeletekisiasa. Ungekuwa hapa kwa Obama mambo yangekuwa mswano sana. Anyway,hata hivyo asante kwa maoni yako, songa mbele bila kuogopa mafisadi.
Mheshimiwa Zitto, I must tell you, I read your message with disappointments, how desperate are you? Huu ni msiba wa taifa na siyo platform ya kujitakatifuza. Meseji yako ni ya kisiasa zaidi na siyo sympathy kwa ndugu zetu waliopoteza maisha na waliopotelewa na ndugu. As a leader you could be somewhere doing something rather than tweeting and facebooking about government and its shortage. GET SERIOUS PLEASE, Kama unavyosema TBC walikuwa busy wanaonyesha taarabu ndio wewe ulivyokuwa busy TWEETING. USHAURI wangu kwako ni kwamba moments like this its better to stick as a family and not pointing finger's (I am sure you know better). Its a about time you guys (oposition parties) starts doing things and stop siasa za kuongelea makosa ya CCM and serikali yake. ITS LOOSING TASTE AND SOON PEOPLE WILL GET BORED
ReplyDeleteMh. Zitto, meongea ukweli kabisa. Lakini tuangalie ukweli ulivyo. Zanzibar sio mkoa wa Tanzania. Ni nchi iliyoungana na nchi nyingine tukatengeneza kitu kama federation. Hata hivyo Wazanzibar hawautaki muungano ndio maana hata mafuta yao wamesema yatolwe kwenye Muungano. Ni wabara ndio hubabaikia Muungano. Kimsingi TBC1 ilitakiwa itangaze habari za msiba kwa vile ni Tv ya Taifa (Zanzibar na Tanganyika). Ila kwa vile Zanzibar hawautaki muungano na wameshasema wao ni nchi kuna haja ya kuangalia mwenendo wao pia kama nchi kwenye matukio kama haya. Ungetupati trend ya matukio na media coverage za Zanzibar. Je vyombo vya habari vya zanziba vilisitisha matangazo yao wakati wa MV Bukoba na Ajali ya Treni Dodoma?
ReplyDeleteWewe acha kutumia Voda wengine tutatumia kama kawa.. Unasahau mchango wa Voda katika elimu na mambo mengine? Susia tuu , utarudi mwenyewe.
ReplyDeleteSUMATRA- huko Zanzibar hakuna?, wawajibike kwanza, wakiongozwa na mkurugenzi wao. Hivi hawa manaodha hizi fani wanzisomea kweli au ndo wanafanya kama dala dala ukiweza kuingiza gia shwali. Kuna maneno yanashindikana kutamkika kwa uzembe wa maksudi kama huu.
ReplyDeleteAlafu viongozi sura zao hazionyeshi huzuni, haya ndo maumbile au nini?
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Yes, I support too. Madaraka, where are you? Do you see this? Do you care?
ReplyDeleteBIG UP ZITO WEWE NI MZALENDO HAKUNA ASIYEJUA HILO UNASTAHILI KUWA RAISI WA NCHI YETU, WANYONGE WATAPIGANIWA HAKI ZAO ZA MSINGI HONGERA SANA, SIKU ZOTE WABINAFSI,MAFISAIDI WANAKUCHUKIA KUTOKANA NA UBINAFSI WAO.
ReplyDeleteWEWE NI GENIUS.
Vodacom imeshiriki mara ngapi katika majanga ya kitaifa leo inahukumiwa??? jamani, kumbukeni Red Alert kipindi cha maafa ya Kilosa, Gongo la mboto nk. nk.
ReplyDeletehuu ni ubaguzi wa wazi dhidi ya Vodacom, napingana na hoja ya kususia huduma zake kisa haikusitisha zoezi la miss tz, miss tz iko chini ya Vodacom ama ni hafla ya kitaifa? na kama waziri anayehusika angesitisha hiyo hafla do u think Vodacom ingekomaa kufanya hilo zoezi siku hiyo?? come on guys, let's be fair to this company. ni mara ngapi wamepeleka michango mbalilmbali katika taasisi tofauti tz bara na visiwani kupitia Vodacom foundation? mna habari kuwa hata suala hili la meli ya znz wamefungua tena Red Alert? do you know what Vodacom is planning to do juu ya suala hili? acheni uvivu wa kufikiria jamani na kuishia kulaumu Vodacom bila kukumbuka mchango wao katika jamii ya kitanzania bila kujali ni maafa ama si maafa! come on guys, let's think positively and wisely. mimi nitatumia Vodacom siku zote ninapotaka kuwasiliana, i wont care propaganda za kutaka kuisusia hata kwa dakika moja.
poleni sana wahanga wa ajali hii mbaya na wote waliofikwa na misiba hii mizito, Mungu wetu awape subira na uvumilivu katika kipindi chote hiki.
ASSALAM ALYKUM
ReplyDeleteNAMUOMBA MUNGU AWAREHEMU WALIOKUFA, NA AWAPE NAFUU WALIOJERUHIWA, NA ATUPE SUBIRA KWA MSIBA HUU.
MUNGU ANAKADIRIA MAMBO KUTOKEA, LAKINI PIA AMEWEKA ADHABU KWA WANAOFANYA MAKOSA. ADHABU AMBAZO ZINAKUSUDIA KUMFANYA BINADAMU AWE NA TAHADHARI KATIKA MATENDO YAKE. KUTENDA, {AU KUTOTIMIZA WAJIBU WAKO} UKASABABISHA MADHARA NI KOSA.
NA TUNAKUWA KUMSUKUMIA MUNGU KWAMBA KAJALIA LITOKEE, SAWA MUNGU KAJALIA, LAKINI PIA MUNGU KAWEKA ADHABU KWA WAKOSA. ILI TUSIWE TUNAENDELEA KURUDIA MAKOSA HAYO HAYO KILA SIKU.
LIKITOKEA JAMBO BAADA YA KUCHUKUA TAHADHARI ZINAZOKUBALIKA, HAPO TUNAMUACHIA MUNGU, NA IKIWA KUNA ALIYEKIUKA TARATIBU, AU KANYAMAZIA KUKEMEA UZEMBE ULIO NDANI YA WAJIBU NA UWEZO WAKE, BASI MUNGU PIA KAWEKA ADHABU KALI.
ADHABU YA MUNGU KUUA MTU MMOJA NI KUULIWA. SASA HAPA WAMEKUFA WATU MAMIA.
JAMANI TUACHE USHABIKI TUZUNGUMZIE JAMBO KWA NJIA YA KUKEMEA UZEMBE.
NAMUOMBA MUNGU ATUSAMEHE MAKOSA YETU. KAMA KUNA LOLOTE KATIKA MANENO YANGU, NI KUTOKANA NA UBINADAMU WANGU.
Haya mambo ya kuiga tamaduni za watu wengi yatatupeleka pabaya. U-miss na kuvaa vichupi si utamaduni wetu jamani!! Utamaduni wa mTZ ni kuwa mtu mkarimu, mwenye kusaidia jamii, jirani akifiwa anaacha yake yote na kwenda mazikoni. Utamaduni wa kiTZ sura wala umbo la mwanamke hazimo katika kuchagua mke wa kuoa. Je leo nchi imo msibani wengine wamepoteza watoto watatu, wengine wamepoteza baba na mama, wewe Lundenga unawaweka watoto wa wenzio mbele ya kadamnasi ya watu na vichupi kuangalia yupi mzuri. U-Miss TZ mwishoooooooooooooooooooooooo!!!
ReplyDeletesawa mheshimiwa umesema tumekusikia. kwa maana hiyo basi mabaa, madisko, na sehemu zote za starehe zingefungwa siku hiyo ili watu wote waomboleze. Kama una uhasama na vodacom watafute siku nyingine utoe donge lako lakini usiwatupie lawama bila sababu maalum. Watanzania kwa ujumla wameshazoea kufiwa ndio maana hawachukulii uzito sana. Asilimia kubwa ya watanzania wamepoteza wazazi wao na ndugu zao wengi sana. Na wakati wao wanalia wengine wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Kufa kupo lakini shughuli nyingine zisisimame. Binadamu tuko tofauti na kila mtu ana moyo wake mwingine ana huruma mwingine hana.
ReplyDeleteTuombe Mola atupe moyo wa kuhurumiana...na awalaze marehemu pema peponi