Ndugu Watanzania mnaoishi Marekani na Mexico,

Napenda kuwataarifu kwamba, kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka nyumbani na kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni kuwa Watu 620 wameokolewa wakiwa hai na watu wapatao 189 wamefariki dunia katika meli iliyozama ya Mv Spice Islanders iliyokuwa ikitokea Bandari ya Malindi Unguja kuelekea Bandari ya Wete Kisiwani Pemba. Huu ni msiba mkubwa uliolikumba Taifa letu kufuatia kuzama kwa meli hiyo katika mkondo wa Nungwi Kaskazini Unguja.

Kufuatia Maafa hayo Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo tarehe 11 Septemba, 2011 na bendera kupepea nusu mlingoti. Aidha, Ubalozi utafungua kitabu cha maombolezo kwa Watanzania siku ya Alhamisi tarehe 15 Septemba, 2011 hadi siku ya Ijumaa tarehe 16 Septemba, 2011 kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania iliyopo 1232 22nd Street NW, Washington DC 20037, saa nne kamili asubuhi (10:00 a.m.) mpaka saa kumi kamili alasiri (4:00 p.m).

Tunawaombea majeruhi nafuu ya haraka. Aidha, tunaelewa machungu ya wafiwa kufuatia msiba huu mkubwa. Mwenyeezi Mungu awape subira, faraja na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Tuzidi kumuomba Mwenyeezi Mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu. Amin.


Mwanaidi Sinare Maajar (Balozi),
Ubalozi wa Tanzania,
Washington, D.C.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...