NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SERIKALI ya Ufaransa imetoa msamaha wa madeni wa mara ya tatu kwa nchi ya Tanzania wa sh. bilioni 9.2 ambapo fedha hizo zitapelekwa katika sekta ya elimu.
Mkataba huo umetiwa saini leo na Balozi wa Ufaransa nchini, Jacques Champagne de Labriolle na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha za Uchumi , Dk. Servacius Likwelile, kwa niaba ya serikali za nchi hizo mbili katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Balozi huyo alisema msamaha wa fedha hizo utapelekwa katika sekta hiyo kwa ajili ya mahitaji ya elimu ya msingi na sekondari.
“ Mkataba huu una sura ya msamaha wa madeni na pia wa maendeleo. Ni sera ya serikali ya Ufaransa kubadilisha fedha zilizolipwa kama madeni kuwa misaada ya maendeleo,” alisema Balozi huyo.
Balozi huyo alisema mkataba wa mara ya kwanza, ulisainiwa mwaka 2003 ulikuwa wa sh. bilioni 5.1 na wa mara ya pili sh. bilioni 7.5, hivyo jumla ya misaada ya Ufaransa chini ya mikataba hiyo ni sh. bilioni 28.
Aliongeza kuwa fedha hizo zote zimepelekwa na zitapelekwa kwenye bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili kuwezesha Tanzania kufikia malengo ya Mpango wa Kukuza na Kupunguza umasikini Tanzania(MKUKUTA) na Millenia.
“Elimu ni sekta muhimu kwa maendeleo. Bila elimu maendeleo hayapatikani,” alisisitiza balozi huyo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Likwelile aliishukuru nchi hiyo , huku akisema msamaha huo utaongeza nguvu ya kuwekeza katika sekta ya elimu.
Wakati huohuo Balozi huyo akizungumzia kuhusu uchumi wa Tanzania, hivi sasa ni bora kuliko miaka iliyopita kutokana na juhudi zinazofanyika za kuwekeza . Pia alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kutokana na jitihada hizo.
LAZIMA WASAMEHE KWA SABABU MGAO KUTOKA LIBYA SIO MDOGO.INASEMEKANA FRANCE WATAPA ASILIMIA 30 YA MAFUTA YA LIBYA KWA KIPINDI NTC WATATAWALA LIBYA.
ReplyDeleteNingependa kuuliza, Deni kwa ujumla tunalodaiwa wa wafaransa ni kiasi gani? Ilituelewe kiasi walichosamehe kinauzito gani. Just imgine kama tunadeni SH Billion 960 alafu wamesamehe Billion 9 tu ni kama asilimia 1. Uandishi wa habari wa haina hii, unaupotoshaji kwa kuwa hauweki fact zote wazi, unataka kumkosha mfaransa. Madeni hayo yalichukuliwa lin? na serikali ipi? kwa lengo gani? na nini kilichofanyika kwa hizo pesa?
ReplyDeleteKama tutakuwa tunapata wadau wenye mtazamo sahihi kama wa huyu anonymos aliyetangulia tutakuwa kidogo kidogo tunapiga hatua kuelekea katika "UELEWAJI SAHIHI WA MAMBO"
ReplyDeleteNi kweli hii habari ya kupunguziwa deni haijakuwa kamili kwa sababu hatujui ni kiasi gani tunadaiwa. Nakubaliana sana tena sana na huyu mdau