ANKAL WAPE WADAU HII WAONE MFANO MZURI WA MRADI WA UJENZI USIO NA MIZENGWE WALA USANII,KONOIKE WAMEWEKA TAREHE YA KUANZA KWA MRADI NA TAREHE WATAKAYO KABIDHI MRADI HUO WA BARABARA. 

HAWA WAKANDARASI WENGINE WANAOGOPA NINI KUWEKA TAREHE YA KUANZA NA KUMALIZA UJENZI KAMA WANAVYOFANYA HAWA KONOIKE...INFACT IPO KWENYE MKATABA WA UJENZI KWAMBA UJENZI UTAANZA TAREHE HII NA UTAMALIZIKA TAREHE HII....

MDAU V. MUSHI WA TEGETA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Sawa kabisa, lakini tunatarajia kuona barabara yenye kiwango cha kimataifa, sio madudu yaliyofanywa Kilwa Road. Tunaambiwa kuwa barabaya hiyo ya Kilwa ilijengwa na kampuni ya Kajima ya Japan, lakini siamini. Barabara hiyo ilijengwa na kampuni ya hapahapa Tanzania baada ya kufanyika usanii mkubwa. Naamini Konoike itatujengea barabara nzuri.

    ReplyDelete
  2. tatizo sio kuandika kwenye kibao, ni kumaliza kwa muda na kwa kiwango kwa mujibu wa mkataba!

    ReplyDelete
  3. Wewe uliyetoa hii picha, fahamu kuwa si Wakandarasi wote wenye matatizo. Kama hapo mwanzo kabisa ingeandikwa kuwa "FUNDED BY TEMEKE MUNICIPALITY" basi huyo mkandarasi angejiuliza mara mia mia kama aandike tarehe ya kumaliza (hata ya kuanza!!)

    ReplyDelete
  4. Kweli anony wa sept 27,12:12:00.Mfano barabara ya ikwiriri hadi lindi inadaiwa kuwa zile km 60 ambazo hazijamaliziwa ni kwamba mkandarasi anaidai serikali malipo yake ya awali, ndio maana unaona hapajengwi na serikali haisemi lolote, hapo kitu kikubwa ni financing tu!barabara ya kilwa ambayo kiwango ni kibovu inapigiwa kelele kwa sababu tu serikali ishalipa pesa yote!

    ReplyDelete
  5. Duh! ni kweli lakini kama ingekuwa funded by Manispaa..Libeneke lingekuwepo, Maana mpk hela ifike kwa mkandarasi ishakatwa katwa sana 10 percent, ikifika kwa mkandarasi lazima ashindwe sema anaanza lini na anamaliza lini, Sababu yeye pia inabidi ile hela aingize kwenye deal zingine kwanza iliapate faida then ndio aanze kazi. Konoike wapo makini sana, Jaribuni kutembea eneo la kazi utaona jamaa wanavyo chapa kazi.

    ReplyDelete
  6. Waandike pia na kiasi cha fedha za wakandarasi(CONTRACTORS) na wasimamizi(CONSULTANTS) wanazotakiwa kupata kila mmoja,hii nayo ni haki ya mtanzania pia.

    ReplyDelete
  7. Kiuhandisi ni jambo la kawaida na la lazima kiutaratibu kuweka bango hilo, uwe makini au bogus lazima uweke.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...