Urban Pulse Creative inawaletea video ya wawakilishi wetu Kutoka Tanzania Linda Kapinga na Lucy Minde katika Bunge la vijana lililoanza tarehe 6-10 Septemba 2011 hapa jijini London. Video hii imefanyika ndani ya ofisi za Ubalozi hapa nchini Uingereza wakati walipopata fursa ya kukutana na Mh Naibu Balozi Chabaka Kilumanga pamoja na baaadhi ya Maofisa wa Ubalozi. Vilevile walifanya Mahojiano maalum na Jestina George kuhusu majukumu pamoja na mtazamo wao kwenye mkutano huu.
Asanteni,
URBAN PULSE  na Miss Jestina Blog 
Ikishirikiana na Ubalozi wa Tanzania Uingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Je hawa vijana walichaguliwaje mpaka wakatuwakilisha TZ kwenye bunge la vijana?

    ReplyDelete
  2. Nimempenda sana Linda. Anajichukulia kama Mtanzania halisi na anajua kujieleza vilivyo bila maringo wala kunata. Lakini huyo mwingine (Lucy) anajifanya mzungu sana, nishai kweli yaani. Mwakilishi gani hata Kiswahili haongei kwa ufasaha kwa kujifanya hakijui? Sipendi sana watu wanaoiga "uzungu uzungu". Jirekebishe mdau.

    ReplyDelete
  3. Big up Urban Pulse Creative. Mnajitahidi sana kwenye utengenezaji wa baadhi ya video zenu.

    ReplyDelete
  4. Simlaumu lucy alivyoongea haonekani kama anaringa au anadharau. Inaonekana haikuwa siku nzuri kwake tu. Kusoma nje kuna stress nyingi jamani tuwe fair

    ReplyDelete
  5. Dada wa media production ame-present vizuri kuliko mwanasheria ingawa kielimu yuko chini ya mwenzake. Balozi wetu uko poa ila fanya mazoezi ya kutamka "th" endapo utamua kutumia lugha za watu, like common wealth na si welsi na mengineyo uliyoyasema. Na wewe TV presenter jitahidi kuwa na mpangilio mzuri kama akina Zainab Badawi na wengineo au ndio umeanza kazi karibuni, anyway mmejitahidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...