Mtakatifu Pope Benedict xvi akihutubia Bunge.

Na Ripota wa Globu ya Jamii.

Kiongozi wa kidini wa kanisa la Kikatoliki duniani Mtakatifu Pope Benedict xvi (Joseph Ratzinger),amejikuta yupo katika mvutano mkubwa na wanasiasa nchini ujerumani,baada ya wabunge wapatao 100 kutoka nje ya bunge la ujerumani wakati Pope Benedict akiwa analihutubia bunge la nchi hiyo (Bundestage) majira ya alasiri ya alhamisi (22-09-2011) mjini Berlin,ambako Baba mtakatifu yupo akiendelea na ziarani nchini hiyo ya Ujerumani.

Wabunge hao walimsusia Pope na kutoka nje ya bunge ambako walijumuhika na waandamaji wa wengine waliokuwa wanampinga Pope kuwepo katika ukumbi huo wa bunge hilo.

Habari za kuaminika na za uhakika zinaeleza kuwa baadhi ya wanasiasa na wabunge nchini ujerumani hawakubaliani na taratibu za uongozi wa Pope ,haswa linapokuja swala la matumizi ya KONDOMU,kwani kanisa la kikatoliki halikubaliani na matumizi ya kondomu,pia sababu zingine za kupingwa kwa Pope nchini ujerumani ni pamoja kashfa zinazowagusa baadhi ya watumishi wa kanisa la kikatoliki duniani kwa kuhusika na kuwafanyia vitendo vichafu watoto au vijana katika miaka ya nyuma.

Pope Benedict amekuwa muwazi na kuwahi mara nyingi kuomba radhi hadharani kwa niaba ya kanisa lake,lakini wakosoaji bado wanaendeleza nongwa ! sababu nyingine ya wanaopinga kulihutubia bunge la Ujerumani ni kuwa DINI NA SIASA ni vitu viwili tofouti kwa maana hii Pope Benedict xvi (Joseph Ratzinger) hapaswi kuwepo ndani ya jumba la bunge au kulihutubia bunge ambalo ndilo baraza la kutunga sheria.

Pope Benedict xvi ni mzaliwa wa Ujerumani,ambapo alizaliwa kwa jina la Joseph Ratzinger ,huko Bayern,Ujerumani ya kusini.

Vyombo vya habari nchini ujerumani vimetonya kuwa kuanzia mwaka 2010 wafuasi wapatao 160,000 wa kanisa la kikatoliki nchini Ujerumani wamelihama kanisa hilo na kujiunga na madhehebu mengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Angekuja TZ wabunge wangegaragara nae na kumpelekea jamaa wao wambusu Pope.

    ReplyDelete
  2. Wabunge wa ujerumani waliomgomea papa,bado sijaelewa sababu zao kuu. madai wanayoyatoa ukitia ndania suala la matumizi ya condom na matatizo ya waathrika wa mnyayaso wa baadhi ya mapadri..issue zote kwaupande wangu ninavyoo fahamu kanisa limeonyesha msimamo dhabiti juu ya hayo mambo mawili,ninachokiona kwa hao wambunge wanalo jambo la siri nalo ni kupingana na kanisa kwamanufaa ya kuutangaza mfumo mpya wa NEW AGES...freedom of thinkng and thought without any boundary (AMBAO UNAENDANA NA SERA YA NEW WORLD ORDER)......Binadamu lazima awe na boundary...

    ReplyDelete
  3. KITU KINACHONIFURAHISHA KWA WAZUNGU KWAMBA NI WA KWELI NA WANA MSIMAMO WAKIAMUA. HICHI KITENDO CHA BAADHI YA MAPADRI WA KANISA LETU KUWAGEUZA WATOTO MAKALIONI KINACHAFUA SANA MSIMAMO WA DINI YETU NA UBINAADAMU KWA UJUMLA. KWA NINI KANISA HALIWI LA KISASA WAPEWE WAKE HAWA HATA KAMA WATAKUWA NI WATU WA MUNGU KAMA WAO. BIBLIA LINASEMA ENEDELEA MKAJAZE DUNIA. WATU WANGELIKUWA MAPADRI NA WAKATOLIKI BASI INGELIKUWA IMEKWISHA WATU.

    ReplyDelete
  4. si unaona wenzetu wajerumani wanavyojua maana ya uwazi na ukweli,kuwa wakweli katika demokrasia yao,Pope angekuja Tanzania wabunge wetu wangejikomba komba na kumbusu

    ReplyDelete
  5. 1. Naomba urekebishe caption, inasema MTAKATIFU... Pope Benedict XVI SIO mtakatifu.

    2. Mchangiaji wa kwanza maoni yako yamekaa "kishabiki" sana, ni ustaarabu na pia vyema kuheshimu imani ya mwingine ikiwa wewe unaamini tofauti.

    3. Mleta habari pia ameiandika "kishabiki" sana akionyesha support kwa kitendo kilichofanywa na wabunge wa bunge la Ujerumani.

    4. About a month ago in Madrid, Spain Pope alikutana na vijana kutoka duniani kote including Tanzania katika hija inayofanyika after every 2 or 3 yrs nothing was posted in blog ya jamii, ila hii ya Bunge la ujerumani ndo imepandishwa faster!!!

    5. Kwa kumbukumbu zangu Jose Chameleon alitoka ukristu na kwenda uislam ilikuwa "breaking news" ndani ya blog ya jamii LAKINI after few weeks akarudia DINI/IMANI yake ya awali yaani Ukristu, nothing was posted here. Si utaratibu mzuri iwapo mlipitiwa/mlisahau katika kutu-update.


    ANGALISHO: Ni hatari Blog ya Jamii ikiingia UDINI - Michuzi naoma ufanyie kazi maoni yangu HATA KAMA hautaipost hii comment nitaelewa Ujumbe Umefika. Kwa kuanza kufanyia kazi haya maoni yangu, hiyo comment ya kwanza IPELEKE KAPUNI.

    Nawasilisha.

    Samweli.

    ReplyDelete
  6. Hahahhhaaaaaaaaa mdau umenichekesha sanaaaaaaaaaaa mwenyezi mungu atuepushe na ushetani huu.Ningeomba ndugu zetu waamke kama wenzetu huko magharibi na kudai haki zao hakuna aibu wala nini kama kunamtu ilimtokea na watumishi hao basi azungumze bayana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...