Wanafunzi wa kitanzania wanasoma katika chuo kikuu cha urafiki (Lumumba) mji wa Moscow nchini Urusi wamefanikiwa kuipeperusha vizuri bendera ya taifa katika medani ya soka katika michuano ya kombe la dunia chuoni hapo baada ya kushika nafasi ya pili katika mchezo wa mkali wa fainali dhidi ya wapinzani  wao wakubwa Ivory Coast iliyopata ushindi wabao 1-0 kwa njia ya penalti iliyotolewa na mwamuzi katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Tanzania ambayo ilionyesha kandanda safi ilionekana kutokuwa na bahati siku hiyo kwani ilikosa magoli mengi ambayo yangeweza kubadili matokeo zaidi.
Michuano hiyo ambayo hujumuisha karibu nchi 20 zikiwemo zile zinazotamba kwa soka Afrika kama Nigeria ambayo safari yao ya mwisho ilikuwa kwa watanzania katika hatua ya robo fainali kwa kufungwa 2-1,na kuwatoa walatino katika pambano la nusu fainali kwa bao 2-1.Nafasi ya 3 ni Guinnea Bissau na 4 ni Walatino.
Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Aisee poleni sana Watanzania wa Moscow. Wenzenu wa Los Angeles wamewachapa Ivory Coast bao 4 kwa 1. Jioneeni wenyewe kwa kugonga hapa : http://www.thehabari.com/habari-tanzania/bongo-starz-yaichapa-ivory-coast-bao-4-kwa-1

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...