Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,Mh Shamsi Vuai Nahodha (kulia) akipokea vifaa maalum kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Richard Wells (katikati), vifaa hivyo vitakavyotumika nchini kote ili kuwapima madereva wanaoendesha magari wakiwa wamelewa.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa kampuni ya Serengeti Breweries (SBL),Teddy Mapunda.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini,Mohamed Mpinga akionyesha baadhi ya vifaa vitakavyotumika kuwapima madereva kiasi cha ulevi wakati wakiendesha magari barabarani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Shamsi Vuai Nahodha akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wanahabari  kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na na kampeni hiyo ya Unywaji wa Pomebe Kistaarabu.Mh Nahodha amesema kuwa takwimu zinaonyesha mwaka 2007 ajali zilizotokea ni 17,617 huku vifo vikifikia 2,838 wakati hasara ya mali ilikuwa ni shilingi Bilioni 508, ambapo makosa ya kibinadamu yaliyosababisha ajali yalikuwa asilimia 176.40%,Aidha Mh. Nahodha ameishukuru kampuni ya Serengeti Breweriers (SBL) kwa kuanzisha kampeni hiyo,ambayo amesema kuwa itasaidia sana kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, Majeruhi na Hasara ya mali nyingi zaidi kwa wanajamii..
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL,Richard Wells akizungumza katika uzinduzi huo mapema leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya serengeti (SBL) Bw. Ephraim Mafuru akifafanua zaidi kuhusiana na kampeni yao waliyoizindua leo,jijini Dar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) ambapo pia walishiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo itakayoanza kutangazwa nchini kote hivi karibuni kwa njia mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ustaarabu upi sasa wa pombe? Pombe inaustaarabu gani? Kweli watanzania tumekosa la kufanya! Tunahamasisha pombe na umeme amna, waziri wa mambo ya ndani lol! Kweli!!?? Tumewachoka jamani! Himizeni mambo ya maendeleo na yanayojenga nchi si uzinduzi na uhamasijaji wa vileo.

    ReplyDelete
  2. Kaka,

    Kwani huyu WAZIRI si MUISLAM huyu au?

    ReplyDelete
  3. Hakuna kitachofanikiwa TZ, kabla ya rushwa kutokomezwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...