Mtoto ambaye hakutambulika jina lake mara moja,anaekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 14-16 akiwa amelala kwenye barabara mara baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Hilux lenye rangi nyeusi,maeneo ya TGNP Mabibo jijini Dar jioni hii.Nambari za usajili za Gari hilo hazikuweza kupatikana mara moja kutokana na mwendo kasi aliokuwa nao dereva wa gari hilo mara baada ya kumgonga mtoto huyo ambaye baadae alikimbizwa hospitali kwa matibabu. 
 Baadhi ya watu waliokuwa wakitoka kwenye kilele cha Tamasha la 10 la Jinsia lililokuwa limeratibiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakikimbilia barabarani kumuangalia mtoto aliegongwa na gari jioni ya leo Maeneo ya Mabibo,jijini Dar.
 Mmoja wa wasamalia wema akiwa amembeba mtoto huyo kumpeleka kwenye gari tayari kwa safari ya kumuwahisha Hospitali ili aweze kupatika matibabu ya haraka.
Kila mtu alikuwa na Shahuku ya kutaka kumtambua mtoto huyo wakati akiingizwa kwenye gari tayari kwa kumkimbiza hospitali ili aweze kupatika matibabu ya haraka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mungu amjalie huyo mtoto apone. Tatizo sheria za Barabara na uvukaji ovyo utizamwe na uendeshaji bila uangalifu pia watu wawe makini.

    TATIZO KUBWA WAGONGAJI WENGI UNAKUTA WAPO AMBAO HAWANA MAKOSA NA WANAPENDA KUSIMAMA NA KUTIZAMA ALIYEMGONGA SEMA KUNA TABIA CHAFU YA WATU KUVAMIA DEREVA NA KUMFANYIA FUJO NA WIZI NA BALAA ZOTE INGEKUWA WATU HAKUNA TABIA KAMA HIZI WENGI PENGINE WANGESIMAMA. MJ

    ReplyDelete
  2. Sawa, usamalia wema ni kitu kizuri sana ila pia unaweza kuwa na madhara makubwa sana kwa muathirika. Huduma ya kwanza ina kanuni zake ambapo, mojawapo, ni namna ya kumbeba mgongwa. Kwa mfano, endapo ajali imemsababishia matatizo ya shingo au mgongo, kisha ukambeba tu kama huyo bwana alivyofanya, unaweza hata kumsababishia kilema cha maisha au hata kifo wakati ni kitu ambacho kingeweza kuepukwa. Hivyo unapoamini unamsaidia mtu unaweza ukawa unamuumiza zaidi au hata kumsababishia kifo. Lakini ndio tufanye nini sasa ukizingatia hali halisi???

    Pole sana mdogo wangu, Mungu akusaidie upone. Naamini aliyesababisha ajali alikimbia kuokoa maisha yake. Lakini kama ni mstaarabu atakuja hospitali kukujulia hali na kukusaidia kadri awezavyo.

    ReplyDelete
  3. Hii picha inaweza kuua sababu kuna uwezekano wazazi, ndugu na marafiki wa karibu hawajapata habari na wanaweza kupata mshtuko mkubwa. Jamani kila mtu ana 'style' yake ya kupashwa habari, tuzingatie sio tu kuwahi breaking news.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...