Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akihutubia Mkutano wa Afrika-Asia 2011 leo ambapo amesisitiza elimu yenye maadili ndiyo njia pekee ya kumkomboa mwanamke pamoja na jamii kwa ujumla. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Wanawake cha Sookmyung nchini Korea Kusini ambacho kimetiza miaka mia moja na tano tangu kianzishwe 1906.
Wahadhiri wa vyuo vikuu, wawakilishi kutoka nchi kumi na mbili za Asia na Afrika (Korea, Tanzania, Bukina Faso, China, Vietinam, Uganda, Nigeria, Senegal, Kyrgstan, Cambodia, Pakistan na Philippine) pamoja na wanafunzi wa Sookmyung wakimsikiliza Spika Makinda.
Spika Makinda akifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa Mkutano iliyotolewa na Rais wa Chuo Kikuu cha Sookmyung, Dkt. Young Sil Han.
Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Korea katika Vyuo Vikuu mbalimbali walifika kumsiliza spika wao.
Baadaye Spika Makinda alipata wasaa wa kukutana na vyombo vya habari na kufafanua umuhimu wa kuwa na vyuo vikuu vya wanawake. Hapa anaongena Avivang Tv ya Korea.
Salma Dinya ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma ambaye alialikwa kwenye mkutano huo kuiwakilisha Tanzania kama kiongozi kijana. Hapa anatoa mada kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Asia na Afrika kuhusu Tanzania.
Rais wa Chuo kikuu cha Sookmyung akitoa maelezo mafupi kwa wageni wake.
Bolozi wa Amani Uingereza Bi Elizabeth B. de. Jong akimkabidhi Spika Makinda zawadi ya kitabu “ Global Citizen”.
Spika akiwa na mazungumzo na watanzania waishio Korea akiwaelezea hali ya nyumbani na kuwaasa wasome kwa bidii na kurejea nyumbani.Picha zote na Prosper Minja –Bunge.
vijana wanaonekana wasikivu..kama sikosei huyo ni Andrew Bukuku mwenye kote la blue...longtime Andrew...Akiko yule mjapani wako tuko naye huku Rochelle New york..anauliza utakuja lini au ndio umetukimbia na kuhamia moja kwa moja Seoul?
ReplyDeleteexperiment naona mzee upo..mzee umetukimbia hata kutuaga..naona kaka zako wanakupa shavu..mmoja kulia mwingine kushoto..aya bwana tukumbukane usitutupe...anyaseyo
ReplyDeletemkurugenzi makina mbona simwoni hapo...au ndio masafari ya fukuoka yamezidi? wewe bukuku mwambie asitusahau huku...tunahitaji ruzuku, ya mwaka jana imeisha mwambie atume nyingine na yale mahoteli ya kitalii wanayotaka kufungua na director mkiba sasa hivi mambo ndio mwake ~mangi~
ReplyDeleteNaona kama sura ya Jitu Athumani Kwikima na Lina Kitosi msikilizeni mama kwa makini sana.
ReplyDeleteBro Kwikima hapo mlikuwa mnaambiwa kitu gani?Naona ulijihisi upo ofisini kwako hapo!Ha ha ha.Masomo mema brother tupo pamoja!!
ReplyDelete