Gari la mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa likiwa limeingia nyuma ya gari ambalo lilikuwa mbele yake kabla ya dereva wa gari hilo la mbele kuamua kurudi nyuma ghafla na kuligonga gari hilo la mbunge.
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (chadema) leo amenusurika katika ajali ya gari baada ya gari lake kugongana na gari jingine ambalo lilikuwa mbele yake kabla ya wa dereva wa gari hilo ambalo lilikuwa likiingia barabara kuu kuamua kurudisha nyuma ghafla gari lake na kuligonga gari hilo na mbunge.

Tukio hilo limetokea leo majira ya mchana wakati mbunge Msigwa akitoka katika kuwatumikia wananchi wake wa jimbo hilo.Hata hivyo katika ajali hiyo gari la mbunge Msigwa halikuharibika sana ukilinganisha na gari hilo lililo rudi nyuma na kumgonga.Picha na Francis Godwin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hivi ninyi mlio nchi za nnje hasa za Magharibi gari za wabunge zina vibendera kama hapa kwetu huko? Na je Ofisi za serikari zina picha ya raisi na madukani kama kwetu hapa?

    ReplyDelete
  2. KITAMBI!!!

    ReplyDelete
  3. Hata mie nashangaa kuona bendera zinapepea ktk magari. Hapa ni viongozi wa juu tu (President na Spika wa Senate na maGoverners) na wakiwa katika safari za kikazi (kumpokea raisi mwingine, kutembelea mikoa na majimbo tofauti etc). Kwa trip za kazini -ofisini hawaweki bendera. Na iwapo kuna bendera basi traffic na SS wanawazunguka.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  4. Mh Mbunge wa CDM nae ana shangingi?

    ReplyDelete
  5. USA na UK hata raia wa kawaida wana bendera, pia magari yao wanaweka bendera. Pia wakienda kwenye michezo washangiliaji pia wana chukua bendera. Bendera ya nchi kuwa nayo sio lazima uwe rais au mbunge bali kila raia anahaki hiyo na hata anaweza kutengenezea mavazi ya ndani!!

    ReplyDelete
  6. napendekeza na wajumbe wa nyumba kumi wapeperushe bendera katika magari yao kama wanayo hayo ndio maendeleo ya uhuru baada ya miaka khamsini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...