Habari ankal,
natumaini hujambo unaendeleza libeneke kama kawa. Mie naomba unifikishie taarifa hii kwa wadau wote wa blog ya jamii na wao wakiweza wawaeleze jamaa zao.


kumezuka wimbi kubwa la madalali matapeli hasa wa nyumba mjini dar wanakuonyesha nyumba hadi jina la mwenye nyumba wanakua wanalijua unaingia hadi ndani kuikagua,ukiridhika nayo wanakupatia namba ya simu ya mwenye nyumba
bandia ukikubaliana nao kila kitu wanadai wanataka kulipwa kwa mwanasheria kwakweli ankal huwezi amini hadi mwanasheria wanakua nae na contract unapewa
na uhakika kwa vile limenitokea inaumiza sana na kurudisha nyuma maendeleo ya watu.


naomba watu wote wawe makini na madalali.
mdau wa blogu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nafikiri hili la mwanasheria ni kuwa mnunuzi pia anatakiwa kuwa naye, hivyo usikubali mwanasheria wa upande mmoja. Hili lilitokea enzi za Mwalim!!

    ReplyDelete
  2. hawa madalali kawasajili nani?

    ReplyDelete
  3. hawa madalali kawasajili nani?

    ReplyDelete
  4. pole sana mkuu. Kuepuka kudhulumiwa wakati mwingine, tembelea madalali wenye leseni za biashara na physical office location.
    Tembelea: www.mydalali.com for more info.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...